KAMPUNI YA NDEGE YA AURIC AIR YAANZA SAFARI MPANDA

Na Walter Mguluchuma, Mpanda Wakazi wa mji wa mpanda mkoa mpya wa katavi  wameanza kupata huduma ya usafiri wa ndege kuanzai juzi Us... thumbnail 1 summary

Na Walter Mguluchuma, Mpanda
Wakazi wa mji wa mpanda mkoa mpya wa katavi  wameanza kupata huduma ya usafiri wa ndege kuanzai juzi Usafiri huo umeanza kupatikana kufuatia kampuni ya ndege ya AURIC AIR kuanza safari ya kusafirisha abiria
Ndege hiyo ya kampuni ya AURIC AIR itakuwa ikifanya safari zake kila siku katika mikoa ya Mwanza, Katavi na Kigoma
Wakazi wa mkoa wa katavi walikuwa wakilazimika kufuata usafiri wa ndege mjini Sumbawanga mkoani Rukwa pindi walipokuwa wakihitaji kusafiri
Uwanja wa ndege wa mpanda ambao ni miongoni mwa viwanja vya ndege vilivyotengenezwa kwa kiwango cha rami toka ulipokamilika ulikuwa haujawahi kutoa huduma ya kusafirsha abiria
Uanzishwaji wa safari za ndege katika mkoa wa Katavi utarahisisha watarii na wawekezaji kufika kwa urahisi mkoani Katavi kwani hapo awali usafiri ulio kuwepo ni wa magari na treni.
Miongoni mwa rasilimali zilizopo mkoani hapa zilikuwa zinashindwa kufikiwa na wageni kutokana na kutokuwa na uhakika wa usafiri wa haraka na wa uhakika
Miongoni mwa rasilimali hizo ni Mbuga ya hifadhi ya Taifa ya Katavi ambayo inasifika kuwa na wanyama wakubwa kuliko hifadhi zote hapa nchini.
Rasilimali nyingine zilizopo ni madini ya aina mbalimbali pamoja na kuwa na sehemu ya ardhi ambayo toka kuundwa kwa ulimwengu haijawahi kutumiwa na binadamu yeyote.