Kilimo cha bangi chaongezeka Burma

Shamba la bangi nchini Burma Umoja wa mataifa unasema kilimo cha b... thumbnail 1 summary
Shamba la bangi nchini Burma

Umoja wa mataifa unasema kilimo cha bangi nchini Burma kimeongezeka kwa mwaka wa sita mtawalia.

Ripoti iliyotolewa na ofisi ya Umoja huo inayoshughulikia masuala ya madawa ya kulevya na uhalifu inasemas sehemu ya ardhi ambayo bangi hiyo imepandwa imeongezeka kwa asilimia kumi na saba.
Umoja huo umelaumu ongezeka la ukuwaji huo wa bangi kutokana na ukosefu wa utulivu na mzozo katika majimbo ya Shan na kachin ambako ndiko kuna mashamba mingi ya bangi.

Inasemekana wakulima hawakuwa na mazao mbadala ya kukuza kando na bangi hiyo ambayo hutumika kama kilewesha kwa kuwa ni zao lenye faida kubwa kifedha.

Burma ni nchi ya pili duniani inayokuza kwa wingi bangi baada ya Afghanistan.

Mwandishi wa BBC anasema hakuna jitihada kamili za kumaliza ukuwaji wa bangi kwa kuwa jeshi nchini humo na makundi ya wanamgambo yananufaika kutokana na biashara hiyo.

Chanzo: BBC