Malengo ya Pambana na
Climate Change ni kukupatia taarifa mbalimbali za mabadiliko ya tabia nchi, mazingira,
maliasili na utalii. Lengo ni kukupatia taarifa sahihi juu ya sababu, madhara
ya mabadiliko ya tabia nchi na hatua muhimu ambazo unatakiwa kuzichukua
kukabilina nayo.
Tusichukulie kuwa
mabadiliko ya tabia nchi ni jambo lisilotuhusu na kwamba linatupotezea muda, la
hasha, mabadiliko ya tabia nchi yanamadhara makubwa sana katika jamii yote. Na
tayari madhara makubwa yameshatokea na kusababisha vifo vya watu wengi na
athari nyingine.
Kwa kuorodhesha madhara
machache yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi ni pamoja na ukame, njaa,
mafuriko, tetemeko la ardhi na kuongezeka kwa joto duniani, magonjwa na
kadhalika.
Hali hii
inatutaka sisi wote kusimama imara kushika silaha na kuanza kupamba na vita hii
ambayo haingoji kesho bali leo, hali hii ya joto duniani sio ya kawaida, kizazi
kijacho kitaungua na kushindwa kuishi.
Kupitia
blog hii utajifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja na namna ya kukabiliana na
mabadiliko ya tabia nchi, pia utapata habari mbalimbali za mabadiliko ya tabia
nchi na mazingira, na kutoa ufafanuzi wa misamiati migumu ya mazingira ili uweze
kupata uelewa wa kutosha juu ya jambo hili.
Pia blog
hii itakupatia njia mbadala za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa
kutumia nishati mbadala na njia nyinginezo ambazo ni rafiki wa mzingira, muda
wa kuandaa mikakati, kujipanga, kuandaa utaratibu umepitwa na wakati na sasa ni
muda wa kutenda, tutende kwa pamoja tutashinda.