MBUNGE AHIMIZA WANANCHI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

Mwandishi wetu, Bukombe MBUNGE wa jimbo  la Bukombe Mkoani Geita, Profesa Kulikoyela Kahigi amewahimiza  wananchi kukabiliana na mabadili... thumbnail 1 summary
Mwandishi wetu, Bukombe
MBUNGE wa jimbo  la Bukombe Mkoani Geita, Profesa Kulikoyela Kahigi amewahimiza  wananchi kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwa kushiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa mazingira.
Profesa Kahigi ameyasema hayo vijiji vya Ibambilo na Isemabuna jana wakati wa mwendelezo wa ziara zake vijijini kuhamasisha maendeleo kwa wananchi na kuelimisha wafahamu jinsi ya kukabiliana na mabadiliko
hayo ya tabia nchi.
Amesema kutokana na mabadiriko ya hali ya hewa
hasa ukame inayolikabili taifa ni vyema wananchi kuanza kulima mazao ya alizeti na muhogo kwa kuwa mazao hayo yanastahimili ukame na kwamba yanaweza kumkomboa
mkulima wa tanzania hasa wa jimbo la Bukombe.
Prof Kahigi asema kuwa mbali na mazao hayo ya muhogo na alizeti kustahimili ukame lakini pia soko lake ni la uhakika na lenye faida kubwa.

Mbunge huyo amewaasa wakulima kuwa sasa inawapasa wachukue hatua ili kukabiliana na mabadiliko haya ya tabia nchi na kuachana na tabia ya kulima mazao ambayo yamekuwa yakiwapa usumbufu kama vile zao la Pamba ambalo bei yake haina uhakika na wamelima miaka mingi bila ya kuona mafanikio.