PICHA 7 ZA HOTELI YA KIFAHARI INAYOTAJWA KUSHIKA NAMBA 1 DUNIANI AMBAYO IPO TANZANIA

HOTELI ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania, inathibitisha kufuru ya utajiri uliopo Tanzania.Singita ndiyo hote... thumbnail 1 summary
HOTELI ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania, inathibitisha kufuru ya utajiri uliopo Tanzania.Singita ndiyo hoteli nambari moja duniani, ikichukua tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na taasisi maarufu ya Marekani, US Travel + Leisure ambayo ‘hudili’ na viwango vya biashara ya utalii duniani.Mmiliki wa hii Hotel ni mmarekani Paul Tudor ambae ameshawahi kuwekwa kwenye list ya mabilionea katika jarida la Forbes na kwenye hii hoteli anashirikiana na Luke Bailes wa Afrika Kusini

 Sasakwa Lodge
  hapa chumbani.

Hii ni moja ya Lodge inayojulikana kwa jina la Sasakwa Lodge iko kwenye kilima kinaitwa Sasakwa Hill. Imejengwa kwa mawe na matofali, juu kwenye paa wameweka bati kisha wakaweka mawe fulani yanapatikana maeneo hayo wao wanayaita "slates".hii yawezekana ndio Lodge  kubwa kuliko zote Hotelini hapo ina vyumba vilivyojengwa kwa mtindo wa "cottages" vipatavyo 15 hivi. 

Taarifa za uhakika ni kwamba kama wiki nne au tano zilizopita waigizaji mastaa wa dunia Angelina Jolie na Brad Pitt walifunga ndoa ya siri na yenye ulinzi kwenye hoteli hii ndani ya lodge ya Sasakwa, watu hawakutakiwa kusogelea wala kamera hazikutakiwa.

 Sabora Plains Tented Camp
Hii ni Sabora Plains Tented Camp, ambayo iko sehemu tambarare kama inavyoonekana kwenye picha. sehemu hii wageni wengi wanaofika  hupenda kupumzika na kuota jua.
Miongoni mwa mastaa ambao mpaka sasa wameshafika kwenye hoteli hii ni pamoja na tajiri wa dunia Bill Gates na baadhi ya washindi wa Olympic 2012
Marais wa 42 na 43 nchini Marekani, Bill Clinton na George W. Bush, kwa nyakati tofauti wamefikia kwenye hoteli hiyo baada ya kuvutiwa na sifa zake zinazotikisa duniani.Bilionea wa Kirusi anayemiliki Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich,alipotembelea nchini Septemba 2009, inaelezwa kwamba alilala kwenye hoteli hiyo.Bilionea wa Kihindi, Mukesh Ambani ambaye kwa sasa ni tajiri namba 19 duniani, alifika nchini mwaka jana na kufikia kwenye hoteli hiyo.

Faru Faru Tented Camp ipo pembezoni mwa Mto Mara.

Angalia hema (tent) linavyoonekana kwa nje kisha angalia ndani kulivyo kuzuri na mpangilio wake ulivyo wa hadhi ya "5 Star Hotel.kiwango cha chini kabisa kulala kwa siku ni USD elfu moja na 50.
 
  Asante sana mybrother "FARI" kwa picha
Chanzo: Ngwesa blog