RUNAPA YAANZISHA UTALII WA USIKU, SASA WATALII KUONA WANYAMA USIKU

HIFADHI ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) imeanzisha utalii wa kuona wanyama nyakati za usiku baada ya kupata kibali cha kufanya hivyo kutoka Shir... thumbnail 1 summary
HIFADHI ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) imeanzisha utalii wa kuona wanyama nyakati za usiku baada ya kupata kibali cha kufanya hivyo kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa nchini TANAPA.
Hifadhi ya Ruaha inakuwa hifadhi ya tatu nchini kuwa na utalii wa aina hiyo wa kuona wanyama wanaopatikana zaidi usiku baada ya hifadhi zingine za Manyara na Tarangile.
Wakiwa kwenye magari maalum na kwa kutumia taa maluum zisizoumiza macho kwa wanyama,watalii watakaofanya utalii huo wa usiku watapata fursa ya kuona wanyama ambao wanapatikana zaidi usiku ambapo Mhifadhi Mkuu wa RUNAPA, Bw.Stephano Qolli amewataka watanzania na walionje ya Tanzania kufika Ruaha na kuona uhalisia wa hifadhi hiyo nyakati za usiku.
Naye Mratibu wa Mradi wa kuimarisha maeneo yaliyohifadhiwa kusini mwa Tanzania,Bw.Godwell ole Meing'ataki na Afisa Utalii Mwandamizi wa hifadhi ya Ruaha,Bi.Eva Pwelle wamesema kuzinduliwa kwa shughuli hiyo ya utalii wa usiku ni moja ya mikakati ya kuboresha huduma katika hifadhi hiyo na kuongeza mapato serikalini.
Mbali na utalii huo wa usiku na vivutio vingine vinavyopatikana Ruaha,hifadhi hiyo pia inacho kivutio cha Msitu mnene wa miyombo ukanda ambao watalii huutumia zaidi kwa utalii wa kutembea masafa marefu na mafupi.
Utalii huo wa kuona wanyama usiku umeanzishwa miezi miwili iliyipota na kwamba kulingana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kugawanyika sehemu mbili za ukanda wa Savana na ukanda wa Miyombo, inabaki kuwa hifadhi pekee nchini yenye wanyama na ndege wengi tofautitofauti.