URAMBO KUTUMIA MISITU KUONGEZA MAPATO YAKE

Mwandishi wetu, Urambo-Tabora HALMASHAURI ya wilaya ya Urambo imejipanga kufanya tathmini yakinifu ya kufahamu thamani ya misitu yake ... thumbnail 1 summary
Mwandishi wetu, Urambo-Tabora

HALMASHAURI ya wilaya ya Urambo imejipanga kufanya tathmini yakinifu ya kufahamu thamani ya misitu yake ili itumike kuongeza thamani ya mali na mapato ya halmashauri hiyo.

Mkuu wa Idara ya maliasili, Ardhi na Mazingira wa halmashauri ya wilaya ya Urambo, Bw.Florence Mwalle, amesema tayari upo umiliki wa misitu lakini kinachokwamisha ni kujua thamani yake.

Amesema hata hivyo anashukuru serikali tayari imefanya utaratibu wa kuthaminisha misitu na baada ya zoezi hilo Halmashauri itajua thamani ya misitu yake na kutumika kuongeza thamani ya mali ilizo nazo Halmashauri.

Halmashauri ya wilaya ya Urambo ambayo sasa ina wilaya mbili za Urambo na Kaliua in Hekta laki tisa na elfu ishirini za misitu huku serikali Kuu ikimiliki Hekta laki tisa na halmashauri ikimiliki Hekta laki mbili na elfu ishirini za misitu.