VIJIJI 12 VYAPATA ELIMU YA KUTUNZA MAZINGIRA KWA UFADHILI FFCS

  Hapa nilikuwa nasoma Taarifa fulani kulingana na huo mradi huku Mratibu wa Asasi hiyo Bw Daudi Masalu akijaribu kunieleza jambo kat... thumbnail 1 summary
  Hapa nilikuwa nasoma Taarifa fulani kulingana na huo mradi huku Mratibu wa Asasi hiyo Bw Daudi Masalu akijaribu kunieleza jambo katika taarifa hiyo
 Bado naendelea kusoma taarifa hizo ili niweze kufanya kazi yangu kwa uhakika
  Wana Kikundi walijumuika nami katika kukamilisha Taarifa hizo
                   Cheti kinajionyesha
 Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr Ally Mohamed Shein ambaye kwasasa ni Rais wa Zanzibar aliwahi kufika katika kikundi hicho na kukagua kama ujuavyo ofisi ya Makamu wa Rais inahusika na Mazingira
Mlima Balili kama unavyoonekana
 
Jamii ya watu wanaozungukwa  na Mlima  Balili uliopo wilaya ya Bunda mkoani Mara wamefaidika na Mradi wa kuwajengea  uwezo kuhusu kutunza Mlima huo ulioandaliwa na Asasi  Lubana Corridor Environmental Development Strategy ya  wilayani humo uliofadhili wa na Taasisi ya The Foundation for Civil Society ya jijini Dar es Salaama kwa mwaka 2009/2010.

Mratibu wa Asasi hiyo Bw Daudi Masalu alisema kuwa Mradi uliokuwa na thamaini ya shilingi zaidi 34 ulikuwa ukivihusu vijiji 12 vilivyokuwa vinazunguka Mlima huo ambavyo ni pamoja na vijiji vya Balili,Bukole,Nyamakoto,yamatoke,Kunzugu,Mihale,Changuge,Mchalo,Ligamba A,Ligamba B,Chilinge na Saragana.

Alisema kukamilika kwa Mradi huo kumeleta faida kubwa katika Asasi hiyo  ikiwa ni pamoja na wanaasasi kupata Mafunzo ya namna ya kusimamia Miradi,kubuni Miradi na kutekeleza Miradi kwa ufanisi mkubwa.

  “Kwa kweli tumenyfaika sana na huu Mradi tuliofadhiliwa na hawa Foundation for Civil Society maana tusingeweza kama wasingekubali kutuwezesha” alisema Bw Masalu

Bw. Masalu alisema kuwa katika kutekeleza Mradi huo Jamii imeonyesha Mabadiliko makubwa ambao kwa pamoja waliamua kuunda Vikundi mbalimbali vya kupanda miti katika Mlima huo,kufuga Nyuki,kubuni Majiko Banifu ambayo yalikuwa mbadala baadala ya kutumia Kuni na kuendelea kuharibu Mazingira ya Mlima huo.

Alisema baaada ya kuendesha Mradi huo kwa Mafanikio makubwa wananchi hao wanaozungukwa na Mlima huo waliamua kuunda sheria ndogo ambazo zilikuwa na lengo la kuulinda Mlima huo usiharibiwe na wananchi waliokuwa wamezoe kufanya vitendo vya kuharibu Mazingira.

 “Baada ya kuutekeleza Mradi huu wananchi walipata ufahamu wa kutosha na kuamua kuunda vikundi mbalimbali vya kuulinda Mlima Balili na kutunga sheria ndogo katika maeneo yao” alisema Mratibu huyo.

Katika kuutekeleza Mradi huo Mratibu huyo alisema kuwa waliweza kushirikisha Makundi mbalimbali ambaayo waliona yana umuhimu wa kufnya hivyo kama vile Walemavu ambao nao waliamua kuanzisha kikundi chao cha kupambana na Umaskini kwa kufanya shughuli ndogondogo kama Ufundi Seremala na hiyo ni baada ya kupata Mafunzo kutoka Asasi hiyo ya Lubana.

Pamoja na kushirikisha baadhi ya Makundi katika Jamii,Bw Masalu aalisema kuwa  Jamii ilishirkishwa kwa kiasi kikubwa katika kufanikisha Mradi huo kama vile kutunza vyanzo vya Maji,upandaji miti,matumizi mazuri ya kuni na kutunza Mazingira ya Mlima huo.

Mbali na hivyo pia Jamii ilishirikishwa katika kubuni MiradiKupanga Miradi huku baada ya sekta na viongozi wa vijiji huska wakialikwa katika semina mbalimbali kujengewa uwezo wa kutunza Mazingira hasa yaa Mlima Balili.

 “ Tumejitahidi sana kushirikisha baadhi ya sekta na viongozi wa Vijiji katika kuwapatia semina na Mafunzo mbalimbali katika utunzaji wa Mazingira na hasa Mlima Balili” alisema Mratibu huyo.

Kuhusu Mahusiano yalipo kati ya Asasi hiyo na Wafadhili wengine tofauti na The Foundatio for Civil Society,mratibu huyo alisema kuwa Mahusiano ni mazuri kuanzia katika Halmashauri ya wilaya ya Bunda na baaadhi ya Taasisi zingine kutoka nje ya nchi.

Alisema mahusiano hayo kuwa Mazuri yanatokana na Asasi yao kujitoa katika kusaidia mambo mbalimbali yanayoizunguka Jamii na hivyo wanajamii kuona umuhimu wa Asasi hiyo huku akitolea mfano Halmashauri kuwaletea baadhi ya Miradi kutoka kwa wafadhili wa nje wanaotaka kusrikiana na Asasi ya wilayani hapoanikisha.

Katika kufanikisha Jambo lolote Mratibu huyo alisema kuwa haliwezi kukosa Changamoto huku akieleza kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa katika kukamilisha Mradi huo ambao mwishoni ulionekana kuleta Mafanikio makubwa kwa wananchi wa Vijiji hivyo 12.

Bw Masalu alisema kuwa changamoto kubwa ilikuwa ni kuwafikia Walengwa kutokana na Jiografia ya eneo hilo la Mlima,wananchi kutokuwae na elimu ya kutosha katika kutunza Mazingira,baadhi ya watu walikuwa wakiishi kwa kutegemea Mlima huo kama chanzo chao cha kujipatia Kipato na Maporomo yaliyokuwa yakitokea katika Mlima huo wakati wa kutekeleza Mradi huo.

 ‘Ndugu yangu kitu chochote  hakikosi Changamoto na katika mradi huu changamoto ilikuwa kubwa kutokana na Jiografia ya Mlim huo yaani ilikuwa tabu sana “ alisema Bw Masalu

Wakiongelea faida walizozipata kutokana na kutekelezwa kwa Mradi huo Bi Mary Mpanda mkazi wa kijiji cha Kunzugu alisemaa kuwa alipata faida kubwa  kutokana na kujua umuhimu wa kutunza Mazingira,kutumia Majiko banifu kwa kuamini kuwa kutumia kuni ni kuendelea kuharibu Mazingira.

 ‘Kiukweli nilipata faida kubwa sana hasa katika suala la kutunza Mazingira na kutumia Majiko Banifu kwani niliona kuendelea kutumia kuni ni kuharibu Mazingira” Alisema Bi Mary

Naye Bi Dotto Bukangi alisema kuwa alinufaika katika suala la kutunza Mazingira,kuziba Makongoro na kutumia Majiko banifu na kufikia Majirani kuona kuwa kuna umuhimu wa kutunza Mazingira.

Aidha akiongelea kuhusu Mradi huo Bi Lidia Mogasa ambaye ni Bi shamba kutoka Halmshauri ya wilaya ya Bunda alisema kuwa Mradi huo umeleta manufaa makubwa kwa Jamii kutokana na Mafunzo yaliyokuwa yakitolewa na Asasi hiyo ambapo Jamii imeonekana kubadilika kwa asilimia kubwa.

  “Ni kweli mradi huo ulitusaidia sana maana Mafunzo tulipata mengi sana na mabadiliko yameonekana katika Jamii yetu katika kutunza Mazingira” alisema Bi Lidia

Katika kuonyesha kufaidika na ruzuku hiyo ya Taasisi ya The Foundation for Civil Society,Bw Masalu alisema kuwa Taasisi hiyo imewasaidia katika kuwajengea uwezo wa kusimamia Mradi,kusimamia fedha,kuhudulia Semina mbalimbali,kuhudhulia katika Maonyesho ya AZAKI mara tatu mfululizo.

Pia Taasisi ya The Foundation for Civil Society imetusaidia kupata vifaa vifaa vya Ofisi huku Jamii ikionekana kuiamini Asasi hiyo kutokana na kuaminika na baadhi ya Taasisi kubwa kama The Foundation for Civil Society.
Chanzo: mwanawaafrika blog