Warembo 16 kati 36 wapatikana katika kushiriki miss utaliii mkoa wa Dodoma‏

Masoud Masasi,Dodoma JUMLA ya washiriki 16 kati ya 36 wamepatikana katika mchujo wa kuwapata washiriki watakaoshiriki katika mashinda... thumbnail 1 summary
Masoud Masasi,Dodoma
JUMLA ya washiriki 16 kati ya 36 wamepatikana katika mchujo wa kuwapata washiriki watakaoshiriki katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa utali kwa mkoa wa Dodoma inayotarajiwa kufanyika Novemba 9 mwaka huu mjini hapa.
Mkurugenzi  wa Island Promotion Tanzania ambao ndio waratibu wa shindano hilo Nyanza Lydenge alisema katika mchujo huo washiriki 16 walipatikana ambao  wataanza mazoezi octoba 13 mwaka huu ambapo amesema watafanya mazoezi kwa kipindi cha wiki tatu kabla ya kuingia rasmi kambini.
Lydenge aliwataja washiriki hao waliopita katika mchujo huo kuwa ni Rachel Kilongo,Jamila Said,Pulcheria Paul,Amina Ayoub,Tibaijuka Leornad,Lightness Kitua,Bertha Patrick,Furaha Kinyunyu,Johan John,Erika Elibariki,Sarafina Jackson,Happy Elias,Sabra Habibu,May Singano,Jesca Peter na Naima Habibu.
“Hawa washiriki 16 tumewapitisha baada ya kuzingatia vigezo vyao tumeridhishwa nao lakini wakati wanafanya mazoezi tutawaangalia pia kwa wale ambao watakuwa na nidhamu mbovu tutawapunguza kwani tunataka mshindi mwenye nidhamu ya hali ya juu”alisema Lydenge.
Alisema washiriki hao katika kipindi hicho watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya mkoa wa Dodoma  katika kuweza kuvitangaza ili viweze kutambuliwa na wadau nchini.
“Wakati wa mazoezi tutawapeleka washiriki kwenda kutangaza vivutio vya utalii  mkoa wa Dodoma ambavyo viko sehemu mbalimbali lakini sisi tutakwenda wilayani kondoa lengo ni kuvitangaza vivutio hivyo mkoani hapa ”alisema mkurugenzi huyo.
Chanzo: Dodoma Yetu