WATU 200 HUUAWA NA WANYAMAPORI KILA MWAKA TANZANIA

Inakadiriwa kuwa watu zaidi ya 200 huuawa na wanyama pori kwa mwaka Tanzania, wanyama hao hatari ni simba, mamba, tembo, viboko, ... thumbnail 1 summary
Inakadiriwa kuwa watu zaidi ya 200 huuawa na wanyama pori kwa mwaka Tanzania, wanyama hao hatari ni simba, mamba, tembo, viboko, fisi na nyoka na kwamba idadi hiyo ya watu kupoteza maisha inaweza kuwa mara mbili ya idadi hiyo huku simba wakitajwa kufanya mauaji hayo kwa asilimia 70.
Mtafiti wa mambo ya wanyama Craig Packer ameeleza kuwa kati ya mwaka 1990 hadi 2004 watu 815 walivamiwa na simba na 563 kuuawa nchini Tanzania.
Wanasayansi kutoka America na Tanzania pia wanaripoti kuwa hali ya binadamu kuliwa na wanyama pori hasa katika maeneo ya vijijini yameongezeka kwa kasi katika kipindi cha mwaka 1990 hadi 2005 ambapo katika kipindi hicho wakazi zaidi ya 500 walipoteza maisha yao kwa kuliwa na simba na kuuawa na wanyama kama tembo.
Idadi hiyo inaonekana kuwa kubwa na kufananishwa na ya karne iliyopita ambapo matukio kama hayo yalijitokeza zaidi katika msitu wa Tsavo.
Matukio hayo yamejitokeza zaidi katika hifadhi ya Selous katika wilaya ya Rufiji, Lindi na maeneo ya mipakani mwa Msumbiji na Tanzania
Pamoja na sababu kubwa ya mauaji hayo kusababishwa na wananchi kuweka makazi katika maeneo ya hifadhi na kufanya shughuli za kila siku katika hifadhi za taifa, lakini wataalamu wanasema kuwa sera za uhifadhi wa mazingira na hifadhi za taifa zinapaswa kutumika ili kupunguza tatizo hili.
Tabianchi