TFDA yachunguza mboga za majani

Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Raymond Wigenge, amesema wanafanya uchunguzi ili kubaini kama mboga... thumbnail 1 summary
Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Raymond Wigenge, amesema wanafanya uchunguzi ili kubaini kama mboga za majani zinazolimwa kandokando ya mito mbalimbali jijini Dar es Salam kama zimeathiriwa na sumu yeyote na kusababisha madhara kwa walaji.

Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam, Wigenge alisema sampuli nyingi za mbogamboga pamoja na vyakula ambavyo havifungashwi, zimechukuliwa kwa ajili ya uchunguzi wa kimaabala na zingine zimepelekwa Ulaya kwa uchunguzi zaidi.

Alisema uchunguzi huo unahusisha maeneo yote yanayohusu vyakula visivyo fungashwa  na baadhi ya dawa zinazotokana na mabaki ya mifugo ili kubaini kama zina madhara kiafya kwa watumiaji.

Aidha, Wigenge, alisema kuwa majibu ya vipimo vya sampuli hizo yatatolewa  Desemba mwaka huu, baada ya kumaliza ukusanyaji na upitiaji wa majibu hayo kutoka maabara ya ndani na nje ya nchi ili kubaini mabaki ya vimelea na madhara yake
 

CHANZO: NIPASHE