Dodoma wataka ‘machifu’ watambuliwe ili kuenzi utamaduni

Chief Mkwawa Mkwavinyika WAKAZI WA KIJIJI CHA BWIBI MKOANI DODOMA WAMEITAKA SERIKALI KUUTAMBUA NA KUTHAMINI UWEPO WA MACHIFU KATIKA M... thumbnail 1 summary
Chief Mkwawa Mkwavinyika

WAKAZI WA KIJIJI CHA BWIBI MKOANI DODOMA WAMEITAKA SERIKALI KUUTAMBUA NA KUTHAMINI UWEPO WA MACHIFU KATIKA MAENEO YAO KAMA NYENZO YA KUENZI TAMADUNI ZA MTANZANIA

WAKIZUNGUMZA KIJIJINI HAPO WANANCHI HAO WAMESEMA WANASIKITISHWA NA UTARATIBU ULIOPO WA KUTOWASHIRIKISHA MACHIFU WAO KATIKA MATUKIO  MBALIMBALI MBALI KILA SIKU

CHIFU WA ENEO HILO LAZARO CHIHOMA AMESEMA KUTAMBULIWA KWA MACHIFU KUTAREJESHGA MAADILI YA KITANZANIA AMBAYO YAMEONEKANA KUTOPEWA NAFASI NA VIJANA NA RIKA NYINGINE HASA MAENEO YA MIJINI


AMETOA MIFANO KWA BAADHI YA VIJANA WA KIMUME KUENDELEA KUSHUPALIA MAADILI YA KIGENI KATIKA MAVAZI NI MOJA YA DALILI MBAYA KATIKA MUSTAKABALI WA UTAMADUNI WA MTANZANIA