Maelekezo I: Unayotakiwa kufanya ukisafiri na ndege kwa mara ya kwanza

Ikiwa ni mara yako ya kwanza kusafiri kwa ndege unaweza kuona ugumu na pengine kuwa na shaka juu ya usafiri wa anga kutokana na kukosa taa... thumbnail 1 summary
Ikiwa ni mara yako ya kwanza kusafiri kwa ndege unaweza kuona ugumu na pengine kuwa na shaka juu ya usafiri wa anga kutokana na kukosa taarifa za kutosha.
Nalazimika kutoa maelekezo haya kwa sababu ni ukweli usiopingika kuwa hakuna mtu anayeweza kukupatia wakati wa safari yako hasa kutokana na watu wengi utakaokutana nao kwenye ndege kuwa na uzoefu wa kusafiri mara kwa mara na kufikiri kila aliyemo ndani naye ni mzoefu.
Mambo ya muhimu kuzingatia wakati unapanga kusafiri kwa ndege ni pamoja na wakati wa kukata tiketi, wakati wa kupaki mizigo yako, nini cha kufanya unapofika uwanja wa ndege, uende wapi, vitu vya kuzingatia wakati wa safari, nanma ya kushughulikia uunganishaji wa safari (kama unasafiri masafa marefu na unahitaji kuunganisha ndege nyingine), wapi pa kuchukua mizigo yako ukifika uendako na kujua swala la usalama wako na mizigo yako.
Wala hupaswi kupaniki, japo kuwa kusafiri kwa ndege kunaweza kukuchanganya kwa mara ya kwanza lakini ukishakuwa mzoefu utaona kila kitu mteremko na kuenjoy safari zako zote.
Sasa wengi wetu huwa hatutaki kujulikana kama ni ma-first time flyers kwa kuogopa kuchekwa, lakini tambua kuwa kila unayemuona kwenye ndege inaweza kuwa ni mara yake ya kwanza kusafiri na ndege hata kama sio lakini naye alikuwa first time flyer wakati anaanza kutumia usafiri huo, kwa hiyo usisite kuuliza wahudumu au hata msafiri mwenzako kwa msaada zaidi.
Baada ya utangulizi huo sasa tuyaone maeneo muhimu wakati wa safari yako ya ndege;

Tiketi; Kuna aina mbili za tiketi za ndege, tiketi za mtandao za elektroniki (e-ticket) na zile tiketi za kawaida (traditional tickets)  hata hivyo mashirika mengi ya ndege siku hzi yanatoa sana tiketi za mtandaoni kutoka na kuwepo mfumo wa kulipa kwa njia ya mtandao.

Ili kupata ticketi yako unatakiwa kuwa na kitambulisho kama vile, leseni ya udereva, kadi ya mpiga kura (kwa wasafiri wa ndani ya nchi) na pasi ya kusafiria (passport kwa wasafiri wanaosafiri nje ya nchi). Njia za kufanya malipo ya tiketi yako ni pamoja na kadi za benki (visa card and master card), kwa Tanzania pia unaweza kulipa kwa kutumia M-pesa, Tigo-Pesa, Airtel-Money na Ezzy Money.

Unachopaswa kujua wakati unakata tiketi

Kuna aina tatu ya madaraja ya tiketi; Economy, Business na First Class na hata haya madaraja pia yamegawanyika kwa namna yake lakini kukibwa ni kwamba kila daraja lina gharama zake kulingana na huduma zinazotolewa kwa abiria akiwa safarini.

Economy; hili ni daraja la chini na hivyo gharama zake za nauli ni ndogo na mara nyingi huduma zake ndani ya ndege zinajumuisha vitu vichache pia

Business and First Class; Haya ni madaraja ya juu ambayo gharama zake za nauli ni kubwa na huduma zake ni nzuri zaidi kwa abiria, ni vizuri kuuliza ni mambo gani utapata ukikata tiketi ya aina hii ili kuona uhalali wa pesa yako.

Una mahitaji maalumu?

Endapo wewe ni mlemvu, unasafiri na watoto na nk, inashauriwa kutoa taarifa hizi wakati ukikata tiketi ili usije kupata shida wakati wa safari yako ukifika.

Unahitaji Chakula maalumu?

Kama tiketi yako inaonyesha kuwa utapata na chakula wakati wa safari yako unahitaji kutoa taarifa ya aina ya chakula unachokula, maana kuna wengine hawali nyama (vegiterians) toa taarifa hizo wakati ukifanya booking ya tiketi yako. Zingatia kuwa sio kila ndge hutoa huduma ya chakula mashirika mengine hayafanyi hivyo.

Unapenda kukaa siti ya dirishani?

Ni kawaida unaweza kuchagua nafasi ya dirishani (kama kuna nafasi), mara nyingi mashirika mengi ya ndege hukupa nafasi ya kuchagua siti wakati wa kukata tiketi yako. Siti za dirishani ni nzuri sana kwa watu wanaosafiri kwa mara ya kwanza kwa maana huwapa fursa ya kuona nje ya ndege lakini wale watu warefu sana ni vyema kukata tiketi ya kwenye korido ili waweze kukaa vizuri.

Ratiba

Iwe unanuanua tiketi yako kwenye ofisi moja kwa moja au kwa njia ya mtandao, omba kupatiwa ratiba ya safari yako, kuna taarifa ndogo lakini muhimu ambazo watu huwa wanajisahau na baade kukutwa na majanga, lazima ujue, ndege inaondokea uwanja gani, muda, reservation number, uunganishaji wa ndege, na kadhalika (mara nyingi e-tickets inakuwa na taarifa hizi zote hivyo ni vizuri kuisoma).

Itaendelea………..