Askari wanyamapori kupewa mafunzo ya kijeshi

Vita ya ujangili na uhifadhi wa wanyama kwa kiasi kikubwa inafanywa na watu wa ngazi za chini yaani walioko kwenye maeneo husika, achana na... thumbnail 1 summary
Vita ya ujangili na uhifadhi wa wanyama kwa kiasi kikubwa inafanywa na watu wa ngazi za chini yaani walioko kwenye maeneo husika, achana na hawa viongozi wetu wanaokaa maofisini na kuagiza hili mara lile, nzungumzia wale askari wanyamapori walioko kwenye hifadhi wanaopurukushana na majangili usiku na mchana.

Hata hivyo idadi ya askari wanyamapori na uwezo wao kimafunzo si yakuridhisha sana katika hifadhi zetu nchini jambo lililofanya kuwepo jitihada za maksudi kuongeza idadi ya askari hao ambapo jumla ya Askari 100 waliofuzu usaili wa awali wa ajira ya uaskari wanatarajiwa kuanza rasmi mafunzo maalum ya mbinu za medani katika hifadhi ya Taifa ya Katavi ili kuongeza nguvu katika idara ya Wanyamapori kukabiliana na vitendo vya ujangiri nchini.

Afisa habari wa Shirika la hifadhi za Taifa TANAPA Paschal Shelutete aanasema kuwa mafunzo hayo maalum ya miezi mitatu kwa askari wake ni utaratibu mpya ulioanzishwa na TANAPA katika kuajiri Askari wakakamavu na wenye mbinu za kuzibiti vitendo vya ujangiri vinavyoendelea hivi sasa.
TANAPA imeandaa mafunzo hayo ili kukabiliana na upungufu wa askari hao lakini pia kuongeza nguvu katika kukabiliana na majangili katika hifadhi za Taifa, mafunzo ambayo yanawalenga askari waliopitia mafunzo ya uaskari katika jeshi la kujenga taifa na chuo cha wanyamapori kilichopo Pasiansi mkoani Mwanza.


Mbali na kuwaimarisha askari wake Shelutete amesema TANAPA kwa kushirikiana na Vyombo vya Dola wameelekeza nguvu katika kuwachunguza na kuwachukulia hatua za kinidhamu na kisheria Wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa wanaobainika kujihusisha na vitendo vya ujangiri.