Baada ya Mwakyembe kufumua mtandao wa dawa za kulenya JNIA, wauza unga wahamia uwanja wa ndege Kilimanjaro (KIA), wanaswa wakisafirisha bangi Uturuki

UWANJA wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) umeanza kutumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kupitisha bangi kwenda nchini Ut... thumbnail 1 summary
UWANJA wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) umeanza kutumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kupitisha bangi kwenda nchini Uturuki.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Kamishna msaidizi wa polisi (ACP), Robert Boaz, aliiambia Tanzania Daima kuwa hivi karibuni walikamatwa watu wawili katika uwanja huo wakisafirisha bangi kwenda mjini Instanbul, Uturuki.
Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Ramadhan Aman (33) mkazi wa Dar es Salaam ambaye alikamatwa hivi karibuni saa 8:30 usiku akiwa na kilo 10.13 za majani ya bangi yakiwa kwenye mabegi.
Kamanda alimtaja mtuhumiwa mwingine kuwa ni Nusura Mtinge mkazi wa Dar es Salaam ambaye alikamatwa saa 9 usiku akiwa kilo 10.1 za majani ya bangi yakiwa kwenye mabegi.
Boaz alisema huo ni utaratibu mpya ambao haukuwepo awali wa kusafirisha majani ya bangi kwenda nchi za nje na kwamba jeshi hilo limeanza uchunguizi ili kubaini mtandao huo.
“Ndani ya miezi miwili tumekamata watu hawa wawili raia wa Tanzania wakitaka kusafirisha bangi, hii inaashiria kuna utaratibu mpya wa kusafirisha bangi nje ya nchi umeanza, tunaendelea na uchunguzi,” alisema.
Wimbi la kusafirisha dawa hizo nje ya nchi kupitia viwanje vya ndege nchini limeshika kasi hususan uwanja wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), hatua iliyomuibua Waziri wa Uchukuzi kulivalia njuga.

Chanzo: Tanzania Daima