Fastjet mmeeleweka!

Nimepokea maoni tofauti tofauti kutoka kwa wadau wa mambo ya usafiri wa anga wakionyesha masikitiko yao kutokana na kusogezwa mbele kwa saf... thumbnail 1 summary
Nimepokea maoni tofauti tofauti kutoka kwa wadau wa mambo ya usafiri wa anga wakionyesha masikitiko yao kutokana na kusogezwa mbele kwa safari ya kwanza ya kimataifa ya ndege ya fastjet kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg wengi wakiwa na wasiwasi huenda shirika hilo linafanyiwa hujuma ili kulipunguza kasi yake ya kutoa huduma bora kwa bei nafuu.

Watu wamesikitika kwa sababu waliipania safari hii ambayo nauli yake ni shilingi 160,000 tu kwa safari moja lakini Kuna neno moja babu yangu alipenda sana kulitumia enzi za uhai wake "Kuchanika kwa jamvi sio mwisho wa maongezi".

Kama hujui mimi mwenyewe nilikuwa miongoni mwa waliotakiwa kufunga mkanda kwenda Bondeni kuwaona jamaa zangu lakini kuahirishwa kwa uzinduzi wa safari hii hakukatishi ndoto yangu hiyo.

Nakumbuka namna jamii ilivyoipokea kwa furaha habari ya fastjet kuanzisha safari za kimataifa kwa bei nafuu ambayo itawezesha maelfu ya wasafiri wa kada mbalimbali kufanya safari zao mara tatu kwa wiki kwenda bondeni na kurudi Tanzania.

Pamoja na fastjet kujipanga vya kutosha na kuonyesha ukomavu katika kutoa huduma za usafiri wa ndege imejikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimika kusogeza mbele safari hiyo ambayo ilipangwa kuanza Septemba 27 mwaka huu kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao.

Katika taarifa yao fastjet wamesema “Uzinduzi wa safari yetu ya kwanza kutokea Dar es salaam kuelekea Johannesburg Afrika Kusini imeahirishwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, tunaomba radhi kwa wateja wetu wote kwa usumbufu uliojitokeza kutokana na tatizo hili"

Fastjet wameomba radhi kwa wateja wake kwa usumbufu uliojitokeza, wamesema WE ARE SORY, nikamsikia na kasuka amerudia maneno hayohayo. Jamani kuna watu wengine kusema samahani wagumu balaa, na kuna wengie kusamehe wenzao ni kazi kwelikweli lakini niseme tu SAMAHANI ni kauli ya kiungwana ambayo inaonyesha kutambua makosa na kuomba radhi ili mambo yaendelee mbele kama kawaida. 

Mimi nimeshawasamehe, nakuomba na wewe ufanye hivyo ili tusonge mbele


By the way fastjet wameahidi kurejesha nauli kwa wateja wote walioathirika na kadhia hiyo "Wateja wote walioathiriwa na mabadiliko haya watarudishiwa nauli zao na kupewa tiketi za bure kusafiri ndani ya mwezi ujao, wanaweza kuwasiliana nasi kwa namba +255 685 680 537 na pia wanaweza kututumia Barua pepe kupitia customer.tanzania@fastjet.com"