HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam inatarajia
kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Baraza la Afrika kuhusu ufumbuzi wa
mabadiliko ya tabianchi, utakaofanyika Oktoba 30, mwaka huu hadi Novemba mosi.
Akizungumzia jana na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, Meya wa jiji hilo, Dk. Didas Masaburi, alisema mkutano huo
unaojulikana kwa jina la ‘International Local Government for Sustainability’
utashirikisha pia Jumuiya ya Tawala za Mitaa, ‘ALAT’.
Alisema kuwa mkutano huo utalenga kukabiliana na
mabadiliko ya tabianchi katika ngazi ya serikali ya mtaa ambayo yanakumbana na
changamoto mbalimbali ikiwamo mabadiliko ya hali ya nchi.
“Nawaomba wananchi wajitokeze kwa wingi ili wajue
athari za kukaa kwenye maeneo mabaya, kujenga miji thabiti na stahimilivu kwa
maendeleo na ustawi wa nchi yetu,” alisema.
Dk. Masaburi aliomba mashirika mbalimbali ya ndani
ya nchi na nje ya nchi kujitokeza kusimamia mkutano huo il ikutoa fursa kwa wao
kujitangaza kibiashara.
Chanzo: Mtanzania