KIKOSI
dhidi ya ujangili kanda ya ziwa(KDU),kimelazimika kwenda katika kijiji cha
Nyamboge tarafa ya Bugando wilayani Geita kuwasaka Fisi wanaodaiwa kuwa tishio
kwa maisha ya binadamu hasa watoto.
Kiongozi
wa kikosi hicho ambaye ni Ofisa wanyama pori wilaya ya Nyang’hwale,Samweli
Mwita,amesema kikosi hicho cha Kuthibiti Ujangili kitakuwa na watu wane wawili
kutoka Mwanza na wengine kutoka wilaya za Geita na Nyang’hwale.
Amesema
hatua hiyo imekuja kufuatia tukio la mtoto,Joshua Pambano(3)mkazi wa Nyamboge
kupoteza maisha kwa kushambuli na kuliwa na fisi.
Mtoto
huyo alinyakuliwa na fisi juzi akiwa Nyumbani kwao majira ya saa 1:30 usiku na
juhudi za wananchi kumpata akiwa hai hazikuzaa matunda baada ya kukuta
ametafunwa na kubaki vipande vidogo vya fuvu la kichwa.
Tukio
hilo ni la pili kutokea kijijini hapo katika kipindi kisichozidi miezi minne
ambapo mwezi wa tano Mwaka huu mtoto Stephano Madeni(2)aliuawa kwa kuliwa na
fisi.
Wanyama
hao wanadaiwa kutapakaa katika makazi ya watu kutokana na Uharibifu wa
mazingira ya Mistu ambapo wamekuwa wakihama kutoka porini kwa kukosa chakula na
kwenda kwenye makazi ya watu.