KLABU YA SOKA YA SUNDERLAND YA UINGEREZA KUWEKEZA KATIKA SEKTA YA UTALII PAMOJA NA KUINUA MCHEZO WA MPIRA WA MIGUU NCHINI

Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw Gary Hutchinson(wapili kushoto)akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es s... thumbnail 1 summary


Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw Gary Hutchinson(wapili kushoto)akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua ya mazungumzo waliyofikia na kujenga kituo cha michezo katika Manispaa ya Ilala ambayo itakuwa chimbuko la kuinua mchezo wa mpira wa miguu(wakwanza kulia)Mkurugenzi wa Michezo Nchini bw.leonard tadeo(wapili kulia)Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki(wakwanza kushoto)Mwakilishi wa klabu ya Sunderland Tanzania,Bw Edmund Hazzad.
Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki.akifafanua kuhusu sekta ya Utalii inafanikiwa na kuinua uchumi wa nchi kupitia michezo Nchini.
Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw Gary Hutchinson,(kushoto)akimkabidhi mkurugenzi wa wizara ya michezo bw.leonard Tadeo.jezi ambao imesainiwa sahihi na wachezaji wa sunderland.
Mkurugenzi wa Mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki(kulia)akimkabizi Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland.Bw Gary Hutchinson,Tisheti ya Bodi ya Utalii.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali walioudhuria kwenye mkutano huo.

SERIKALI imesema ipo katika hatua za mwisho za mazungumzo na uongozi wa klabu ya soka ya Sunderland ya Uingereza ili kuwekeza kwenye maendeleo ya sekta ya Utalii pamoja na kuinua mchezo wa mpira wa miguu nchini.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Uwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Dk. Aloyce Nzuki alisema lengo la kufanya hivyo ni kutafuta wawekezaji wa kuhakikisha sekta ya Utalii inafanikiwa na kuinua uchumi wa nchi kupitia michezo.

Alifafanua kuwa tangu kuanza kwa mazungumzo hayo Tanzania imeanza kunufaika kwa kuwa na ongezeko la watalii la asilimia 30 hali ambayo inaonekuwa kuwepo kwa mafanikio yanayohitajika.

Alisema Uingereza ndio nchi inayoongoza kwa utalii nchini na kwamba uwekezaji huo unalenga kuinua pato la nchi kwa kuongeza ukuaji wa uchumi na kupunguza umasikini.

"Vivutio vya Tanzania vinaoneshwa kupitia Uwanja wa timu hiyo nchini Uingereza katika michuano ya Ligi Kuu ya huko inayoonekana na mashabiki wengi duniani na kutoa fursa na hamasa kuja nchini kutembelea vivutio vyetu na kuongeza uchumi wa nchi," alisema.

Pia Dk. Nzuki aliushukuru uongozi wa klabu ya Sunderland kwa kuendeleza ushirikiano katika kuinua utalii wa Tanzania kupitia sekta ya michezo kitu ambacho kila mdau anasubiri mafanikio hayo kwa hamu kubwa ili Tanzania ifanye vema katika mashindano ya kimataifa.

Wakati huo huo Mkurugenzi wa Biashara wa klabu ya Sunderland Gary Hutchinson, alisema moja ya hatua ya mazungumzo waliyofikia na kujenga kituo cha michezo katika Manispaa ya Ilala ambayo itakuwa chimbuko la kuinua mchezo wa mpira wa miguu.

Licha ya kujenga kituo hicho cha michezo (Academy), watajenga uwanja wa kisasa wa michezo utakaokuwa moja ya sehemu ya uwekezaji katika sekta ya michezo itakayoleta maendelea katika nyanja hizo na kufikia mafanikio kwa ushirikiano na kampuni ya Marekani ya Simbion.

"Tutaanzisha kituo cha michezo (Academy) katika eneo la Kidongo Chekundu wilayani Ilala, Dar es Salaam ambayo itasaidia kutangaza utalii kimataifa kupitia sekta ya michezo na kufikia mafanikio yanayohitajika," alisema.

Mkutano huo wa waandishi wa habari ulihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Sunderland pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Michezo ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamduni na Michezo.