Mkurugenzi
idara ya mazingira ofisi yamakamu wa Rais Dkt Julius Ningu akisoma hotuba ya
ufunguzi katika maadhimisho ya siku ya kimaifa ya hifadhi ya tabaka la ozone
inayofanyika kitaifa mjini mwanza leo.
Na Evelyn Mkokoi
Imelezwa kuwa kuharibiwa kwa tabaka la ozoni husababisha
kuongezeka kwa magonjwa, kama vile saratani ya ngozi, uharibifu wa macho kama
vile "mtoto wa jicho" unaosababisha upofu, na upungufu wa uwezo wa
mwili kujikinga na maradhi.
hayo yameelezwa leo Jijini Mwanza na mkurugenzi wa idara ya mazingira kutoka
ofisi ya makamu wa rais Dkt Julius Ningu katika kilele cha maadhimisho ya siku
ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la ozoni.
Picha
ya pamoja ya washiriki wa warsha katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya
hifadhi ya tabaka la ozone inayofanyika kitaifa mjini mwanza leo.picha na
habari na (Evelyn Mkokoi)
Dkt. Ningu amesema kuwa
watoto wako katika hatari zaidi ya kupata madhara haya, na madhara
mengine katika viumbe hai, pamoja
na kuharibika kwa fiziolojia ya mimea na
utaratibu wa ukuaji wake.
Dkt Ningu ameendelea kusema kuwa, madhara haya yanaweza
kuchangia mabadiliko katika muundo wa spishi, hivyo kuathiri bioanuwai katika mifumo ikolojia mbalimbali,
na yaweza kuchangia kuathiri uzalishaji, ukuaji na uwezo wa kuzaliana wa viumbe
wa majini, na uharibifu wa vifaa
mbalimbali vya aina ya plastiki.
Awali akifungua mafunzo kwa washiriki ikiwa ni sehemu ya
kazi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la ozoni,
Mgurugenzi msaidizi osifi ya kamau wa rais mazingira bi Magdalena Mtengu
amesema kuwa kumong’onyoka kwa tabaka hilo kutokana na mlundikano wa gesi aina
mbali mbali.
alitolea mfano wa gesi hizo kuwa kuwa
ni pamoja na, chloroflourocarbons
(CFCs), halons, methyl choroform, methyl
bromide, carbon tertrachoridena ambazo
ni sehemu ya kemikali zinazotumika katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya
kuzimia moto, ushafishaji chuma, utengenezaji wa magodoro, madawa na manukato
ya kupulizia, ufukizaji wa udongo katika vitalu vya tumbaku na mashamba ya maua
na upiliziaji wa madawa kwenye mazao katika maghala.
Na Ili kunusuru
uharibifu wa tabaka la ozone na madhara yake kwa viumbe hai na mimea serikali za
jumuiya ya umoja wa kimataifa kwa pamoja ziliridhia Mikataba mbali mbali
ukiwemo wa Montreal wenye lengo la kudhibiti
utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka hilo.
maadhimisho haya kitaifa mwaka huu yanafanyika mjini
mwanza yakiwa na malengo ya kutoa mafunzo kwa mafundi, wenye viwanda na elimu
kwa wananchi kupitia vyombo vya habari.