MAADHIMISHA YA SIKU YA KIMATAIFA YA HIFADHI YA TABAKA LA OZONI KUFANYIKA SEPTEMBER 16 2013.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano kushoto mh. Samia suluhu Hassan kwa Niaba ya waziri wa nchi wa nchi Ofisi ya makamu wa Ra... thumbnail 1 summary
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano kushoto mh. Samia suluhu Hassan kwa Niaba ya waziri wa nchi wa nchi Ofisi ya makamu wa Rais Mazingira Dkt Terezya Hufisa, akisoma hotuba kwa waandishi wa habari hawapo pichani kuelekea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya hifadhi ya tabaka la Ozone, ambayo huadhimishwa kila mwaka Sepetember 16 kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt Julius Ningu (Picha na Ofisia ya Makamu wa Rais)

Na Evelyn Mkokoi & Rashda Rashid
Ili kufanikisha utekelezaji wa mkataba wa Montreal, serikali imeandaa na kutekeleza programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu kwa tabaka la ozoni.

Akiongea kwa Niaba ya ya waziri wanchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira waziri mwenye dhamana ya kushughulikia masuala ya Muungano Mh. Samia Hassan Suluhu alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, amesema mikakati ya kitaifa ndani ya Programu hii ni pamoja na kujenga uwezo wa taasisi zinazosimamia utekelezaji wa mkataba, kutoa elimu kwa wadau na umma wa watanzania kuhusu umuhimu wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili.

Mheshimiwa suluhu aliongeza kwa kusema kuwa kubadilisha technolojia katika viwanda vinavyotumia kemikali haribifu na kutoa mafunzo yanayolenga kuimarisha ujuzi katika sekta ya kuhudumia  viyoyozi na majokofu na kuhamasisha na kuhimiza matumizi ya kemikali na technolojia mbadala na rafiki kwa tabaka la Ozoni ni njia ambazo serikali inatumia kunusuru kuharibika kwa tabaka la hewa ya Ozoni

 “Ni muhimu tuzingatie kwamba juhudi za kila mmoja wetu zinatakiwa kupunguza na kuondosha mathara katika Tabaka la Ozoni yanayo sababishwa na bidhaa tunazo nunua na kutumia majumbani au sehemu za biashara alisisitiza.”

Mh Suluhu aliwaasa wananchi kushiriki katika kuhifadhi Tabaka la Ozoni kwa kuzingatia  kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku, kuepuka kutupa ovyo majokofu na viyoyozi chakavu ama vifaa vya kuzuia moto vyenye kemikali zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni,
Alitoa wito kwa mafundi wa majokofu na viyoyozi waakikishe kuwa wananasa kwa kutumia tena vipoozi  (refrigerants) kutoka kwenye viyoyozi, na majokofu wanayo hudumia badala ya kuviachia huru ili visisambae angani na amewashauri mafundi hao watoe elimu kwa wateja wao juu ya njia raisi za kutambua uvujaji wa vipoozi.

Maadhimisho hayo ya siku ya Ozoni duniani ambayo huadhimishwa tarehe 19 ya mwezi wa September kila mwaka, mwaka huu yatafanyika katika chuo cha VETA-Nyakato jijini Mwanza yakiambatana na maonyesho ya bidhaa na technolojia mbadala na rafiki kwa Tabaka la Ozoni Pamoja na mafunzo na njia bora za technologia sahahi ya kuuudumia viyoyozi, majokofu na mitambo ya kupoozea viwandani

Walengwa wakubwa wa maadhimisho haya ni mafundi wa kuudumia majokofu viyoyozi mitambo ya kupoozea kutoka viwandani vya kusindika minofu ya samaki vinywaji na taasisi za ufundi zenye fani ya kuudumia majokofu na viyoyozi. Lengo kuu ni kuelimisha mafundi kuhusu technolojia mpya.