MAADHIMISHO YA KILELE CHA SIKU YA UTALII DUNIANI YAFANA JIJINI MWANZA

Tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ni Siku ya Utalii Duniani ambapo sherehe hizi hufanyika duniani kote. Mwaka huu, Siku ya Utalii Duniani ki... thumbnail 1 summary
Tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ni Siku ya Utalii Duniani ambapo sherehe hizi hufanyika duniani kote. Mwaka huu, Siku ya Utalii Duniani kitaifa iliadhimishwa Jijini Mwanza ambapo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Lazaro Nyalandu alikuwa mgeni rasmi.
 Mhe Lazaro Nyalandu akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kufungua rasmi ofisi mpya ya Bodi ya Utalii Tanzania Kanda ya Ziwa
Mhe. Lazaro Nyalandu akipata maelezo kutoka kwa mtumishi wa Marine Parks and Reserves
 Mhe. Lazaro Nyalandu akifurahia taswira ya mnyama aina ya simba aliyekuwa katika banda la Wizara ya Maliasili na Utalii

Maadhimisho haya yalipambwa na shughuli mbalimbali ikiwemo ufunguzi wa ofisi mpya ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Kanda ya Ziwa. Ofisi hii imefunguliwa ili kukidhi mahitaji ya utangazaji wa utalii kwa Kanda ya Ziwa. Aidha, shughuli nyingine kuu ya ofisi hii ni kuhamasisha utalii kwa wananchi wa Mwanza na pia kuanisha vivutio vipya ya utalii na kuvitangaza.

Mhe Lazaro Nyalandu akipata maelezo kutoka mtumishi katika banda la Wizara ya Maji

Akizungumza katika kilele cha Siku ya Utalii Duniani, Mhe Lazaro Nyalandu aliwaasa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujenga utamaduni wa kutembelea vivutio vya utalii na kushangaa nchi yao. Akitumia maneno yaliyomo kwenye wimbo wa ‘Nakupenda Tanzania’ yasemayo “Tanzania Tanzania ninapokwenda Safarini, kutazama maajabu” alisema wimbo huu uliotungwa na wazee wa zamani ulionyesha hazina kubwa ya vivutio vilivyopo nchini na hivyo kuhamasisha utalii kwa wananchi wote.
Mhe Lazaro Nyalandu akiangalia kazi za mikono ya kikundi cha utamaduni kutoka Mugumu.
Sherehe hizo pia zilipambwa na burudani ya ngoma za asili kutoka kikundi cha utamaduni cha Bujora. Pamoja na ngoma hizo, mabanda yaliyofanya vizuri katika maonyesho haya yalizawadiwa ambapo Wizara ya Maliasili na Utalii illibuka mshindi wa kwanza, ikifuatiwa na Wizara ya Maji na ya tatu ilikuwa Hoteli ya J.B.Belmont ya Jijini Mwanza.
Wengine waliozawadiwa ni wanafunzi wa shule ya sekondari ya Kirumba waliofanya vizuri katika mashindano ya insha inayohusu utalii. Washindi hao ni Zuberi Kihumbe wa Kidato cha Pili, wa pili ni Mariam Shabani wa Kidato cha Pili na wa tatu ni Renatus Leonard wa Kidato cha Tatu.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Lazaro Nyalandu alitoa rai kwa wananchi kuwekeza kwenye sekta ya utalii kwani takwimu zinaonyesha kuwa kati ya kazi kumi duniani moja ina uhusiano wa moja kwa moja na utalii. Aliwashauri kuitumia ofisi ya TTB ili kujielimsha juu ya fursa mbalimbali za utalii zinazopatikana Kanda ya Ziwa.