Miss Utalii kushiriki mashindano ya dunia

MSHINDI wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hadija Mswaga, ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro, anatarajiwa kwenda nchini E... thumbnail 1 summary
MSHINDI wa taji la Taifa la Miss Utalii Tanzania 2012/2013, Hadija Mswaga, ambaye pia ni Miss Utalii Morogoro, anatarajiwa kwenda nchini Equatorial Guinea Septemba 28, mwaka huu ,kushiriki mashindano ya Dunia ya Miss Utalii.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Habari na Masoko wa Miss Utalii Tanzania, Fredy Njeje, fainali hizo zitafanyika Oktoba 12, kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Sipopo Conference Centre, Malabo Equatorial Guinea. 

Jumla ya washiriki kutoka nchi 126 duniani watashiriki katika mashindano hayo, ambayo mwaka jana yalifanyika nchini Thailand ambapo mrembo Tatyana Maksimova wa Urusi alishinda taji hilo.

Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Tanzania kushiriki mashindano hayo ya Miss Utalii Dunia, ambapo kila mwaka kuanzia mwaka 2005 tumeshinda mataji, mataji hayo na washindi kutoka Tanzania katika mabano ni Miss Tourism World 2005- Africa (Witness Manwingi- Tanzania), Miss Tourism World 2006-SADC (Killy Janga - Tanzania), Miss Tourism World 2007- Africa (Lillian Cyprian- Tanzania), Miss Tourism World 2008- Internet (Lilly Kavishe- Tanzania) na Miss Tourism Model Of The World 2006-Personality (Witness Manwingi- Tanzania). 

Tangu mwaka 2008, Tanzania haikushiriki katika mashindano hayo, kutokana na kukosa wadhamini wa safari hizo na matatizo mengine ya kiufundi, ikiwemo kutofanyika kwa mashindano hayo nchini kuanzia 2008 hadi 2010.


Chanzo: Mtanzania