MZEE ANDENGENYE MALLANGO: KAZI YA ULINZI WA MALIASILI INAHITAJI UJASIRI NA MOYO WA UZALENDO NA SIO TAMAA

               ANDENGENYE MALLANGO Akifafanua jambo. Aliyekuwa Afisa Maliasili na Mazingira wilaya ya Morogoro Andengenye Mallango amewata... thumbnail 1 summary
               ANDENGENYE MALLANGO Akifafanua jambo.

Aliyekuwa Afisa Maliasili na Mazingira wilaya ya Morogoro Andengenye Mallango amewataka vijana kutokubali kurubiniwa na fedha za majangili bali wawe wazalendo kwenye kuhakikisha maliasili za taifa ili zidumu vizazi kwa vizazi.

Mallango ameyasema hayo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na watoto wake kwaajili ya kumshukuru Mungu na kumpongeza kwa kuweza kumaliza utumishi wake serikalini kwa amani na salama.

Akishukuru wakati wa hafla hiyo amesema kuwa kazi ya ulinzi wa maliasili unahitaji moyo na uzalendo kutokana na majangiri wengi kuwa tayari kufanya lolote kuokoa maisha yao na kukwepa kukamatwa, amesema wengi hutumia fedha na vitisho ili kutimizz adhma yao lakini katika utumishi wake amefanikiwa kusimamia maadili na misingi ya kazi yake kwa nguvu zake zote.


Chanzo: Gwabalajrblog