Njombe wafurahia uzinduzi wa safari mpya za ndege za Auric Air mkoani humo

( Habari hii inakujia kwa udhamini wa Auric Air ) Sekta ya usafiri wa anga inazidi kukua kila kukicha ambapo mashirika mbalimbali ya ndeg... thumbnail 1 summary
(Habari hii inakujia kwa udhamini wa Auric Air)
Sekta ya usafiri wa anga inazidi kukua kila kukicha ambapo mashirika mbalimbali ya ndege yanaendelea kutanua huduma zake katika mikoa mingi hapa nchini.
Abiria muda mfupi baada ya kutua katika uwanja wa ndege wa Njombe

Septemba 16 mwaka huu Auric Air imezindua safari yake mpya ya Dar es Salaam kupitia Iringa kwenda Njombe ambapo sasa wakazi wa Njombe na maeneo ya jirani watanufaika na usafiri wa haraka na salama unaotolewa na shirika hilo.
Nani asiyependa kujinafasi? nani asiyependa ku-enjoy? jibu ni wote na mafanikio haya yatakuwa chachu kubwa katika maendeleo ya Njombe na maeneo ya jirani.


 Ndege ya Auric Air ikiondoka kwenye uwanja wa ndege wa Njombe