NYARANDU KUPOKEA MAANDAMANO YA KUPINGA UJANGILI WA TEMBO NCHINI

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) anatarajia kupokea Maandamano ya Kupinga Ujangili wa Tembo yaliyopewa jina ... thumbnail 1 summary

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) anatarajia kupokea Maandamano ya Kupinga Ujangili wa Tembo yaliyopewa jina la ‘Tembea kwa ajili ya Tembo’ ambayo yanatarajiwa kuwasili Jijini Dar es Salaam kesho tarehe 12 Septemba 2013 majira ya asubuhi. Maandamano hayo yamechukua muda wa siku 19 na waandamanaji wametembea kilomita 650, kutoka Jijini Arusha.
Matembezi hayo ya kupinga ujangili yameandaliwa na Taasisi ya African Wildlife Trust (AWT) yakiwa na lengo la kuelimisha wananchi na Ulimwengu mzima kwa ujumla juu ya madhara ya ujangili. Matembezi yamehusisha raia wa nchi mbalimbali duniani.
Mhe. Lazaro Nyalandu (Mb) ambaye ndiye mgeni rasmi katika kilele cha matembezi hayo anatarajiwa kuungana na msafara wa waandamanaji eneo la Ubungo Jijini saa tatu asubuhi na kutembea nao hadi viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo atapokea risala kutoka kwa waandamanaji.