MSANII
wa muziki wa asili Saida Karoli juzi ameibuka mshindi katika tamasha la ni nani
zaidi, kati ya wasanii wote ambao wamerekodi kazi zao katika studio ya Tivol ya
jijini Mwanza.
Tamasha
hilo lilifanyika katika uwanja wa karume mjini Musoma na kuhudhuriwa na
wananchi zaidi ya 5,000 kutoka maeneo mbalimbali mkoani humo.
Murugenzi
mtendaji wa studio ya Tivol, Nilivinus Madaraka, jana alisema kuwa katika
tamasha hilo, Saida Karoli aliibuka mshindi, akifuatiwa na Bhudagala
Mwanamalonja na nafasi ya tatu ilishikiliwa na Papaa Kishapu.
Madaraka
alisema kuwa tamasha hilo lilishirikisha wana muziki 16 ambao wote kazi zao
zimerekodiwa katika studio yake na kwamba lengo lake lilikuwa ni kuutangaza
muziki wa asili na kuenzi mila na utamaduni wa mtanzania.
Aidha,
alisema uwa katika tamasha hilo wasanii walipiga miziki ya asili ili kudumisa
utamaduni na mila za mtanzania na kwamba kulingana na idadi kubwa ya watu
walioingia zilipatikana zaidi ya shilingi milioni nane.
Alisema
kuwa jumamosi ijayo Saida Karoli atatumbuiza katika mji wa Bukoba kwenye ukumbi
wa Linaz Club na jumapili atakuwa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini humo.