Picha halisi za wanyamapori zilizopigwa kwa mpangilio utadhani zimetengenezwa kwa photoshop

Kadri siku zinavyokwenda teknolojia nayo inazidi kuchukua hatamu yake kiasi ambacho mtu sasa anaweza kufanya miujiza ya namna mbalimbali ka... thumbnail 1 summary
Kadri siku zinavyokwenda teknolojia nayo inazidi kuchukua hatamu yake kiasi ambacho mtu sasa anaweza kufanya miujiza ya namna mbalimbali katika picha na kuifanya ionekane atakavyo yeye akisaidiwa na software tofauti tofauti ikiwemo photoshop au adobe. 
Lakini amini usiamini, kwenye ulimwengu wa utalii na mambo ya wanyamapori barani Afrika hakuna anayepoteza muda mwingi kuphotoshop picha na matukio ya wanyama hao maana wengi wa wanyamapori wa huku kwetu huonekana kwenye kamera wakiwa katika muonekano mzuri ambao ukiuangalia unaweza kudhani ni photoshop imefanya kazi yake.
Source
Watu wenye mapenzi mema wameshare picha nane za wanyama ambao walipigwa picha wakiwa katika mapozi yatakayokufanya hata wewe uhisi photoshop ime take place!
Picha hizo ambazo zimepatikana kwenye ukurasa wa facebook ya Africa, this is why I live here, zimeambatana na maneno haya "In Africa, we don’t need photoshop – our animals just do it for us!"
Pata fursa ya kuona picha zenyewe na ukimaliza usisite kuacha comment yako hapo chini