Picha: Mtoto wa chui akicheza na kakakuona mchezo wa paka na panya

Mtoto mchanga hupenda kujifunza kwa kujaribu kufanya mambo mengi, mengine ya hatari lakini lengo lake ni kujua mambo, ndivyo ilivyotokea kw... thumbnail 1 summary
Mtoto mchanga hupenda kujifunza kwa kujaribu kufanya mambo mengi, mengine ya hatari lakini lengo lake ni kujua mambo, ndivyo ilivyotokea kwa mtoto wa chui wa mwaka mmoja ambaye baada ya kukutana na kakakuona cha kwanza ilikuwa ni kushangaa na kuanza kucheza nae kama paka na panya.

pangolin_3
Mnyama huyu adimu kuonekana ambaye pia inaaminika (katika baadhi ya tamaduni) kuwa kuonekana kwake kuna ashiria bahati nzuri kwa mtu au taifa fulani, ameonekana katika hifadhi moja huko Batswana akiwindwa na mtoto wa Chui. unajua nini kilichotokea? Chui huyo aliishia kushangaa tu asijue la kufanya. Hii inatokana na tabia ya kakakuona ya kujivingirisha na kutengeneza umbo la mpira hivyo kuzuia mashambulizi ya aina yeyote kutoka kwa wanyama wakali
pangolin_1x
pangolin_leopard6
pangolin_3x
Nimefanya utafiti mdogo kwennye vyanzo kadhaa vya habari za mambo ya utalii na inaonyesha kuwa zaidi ya miaka 10 imepita bila kutokea kwa tukio kama hili nchini humo (Botswana) lakini kama kuna mtu atakuwa amewahi kushuhudia tukio kama hili kwa hapa Tanzania na sehemu nyingine za dunia karibu kushare nasi habari na picha pia.
pangolin_leopard12pangolin_leopard5
pangolin_2
pangolin_leopard11
pangolin_4x
Katika mkasa huu kakakuona alikuwa akijiviringisha kwa muda na baada ya kuona kimya anajiachia na kuanza kutembea lakini chui aliendelea kumparua na makucha yake. na wakati mwingine alimn'gata japo alikunja sura kama kuonyesha uchungu au kuumizwa na magamba ya kakakuona.
pangolin_leopard9pangolin_leopard8pangolin_leopard2pangolin_leopard1
Imeandaliwa na tabianchi kwa msaada wa mtandao wa Geographic