Picha na Maelezo: Mamba ajificha chini ya uvungu wa kitanda ndani ya hoteli ya kitalii

Unaweza kudhani ni ndoto ama simulizi ya kusadikika lakini tukio hili la ajabu limetokea kweli baada ya mamba mkubwa mwenye futi 8 kuingia ... thumbnail 1 summary
Unaweza kudhani ni ndoto ama simulizi ya kusadikika lakini tukio hili la ajabu limetokea kweli baada ya mamba mkubwa mwenye futi 8 kuingia chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa Hoteli ya kitalii ya Humani iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini Zimbabwe na kukaa zaidi ya masaa 8.

Sipati picha kama wewe ndie ungekutwa na mkasa huo ingekuwa hatua yako ya kwanza kuchukua, (najua mbio zake!!! Usain Bolt angeshika adabu). Hata hivyo mkurugenzi wa hoteli ya Humani, Mr Whittall anaeleza namna mamba huyo alivyoingia kimya kimya chumbani kwake na kukaa chini ya kitanda chake usiku na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata.

Mamba chini ya uvungu??? tazama picha zake

Utajiuliza mamba huyo alitokea wapi hadi kuingia ndani ya chumba cha hoteli hiyo lakini maelezo ya Mkurugenzi yanaeleza kuwa huenda mamba huyo alitokea nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo ambapo hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake huku mamba huyo akiwa chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa hoteli hiyo.

Habari zaidi zinasema mamba huyo aligunduliwa na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi katika chumba hicho na kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo alitoka mbio mithiri ya digidigi kwenda kushuhudia kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa chini ya kitanda chake. Hah! kumbe alilala naye kwenye chumba hicho usiku mzima.

"Mamba ni wataalam wa kujificha na ndiyo maana hunusirika kuuwawa na wanyama wengine hususani binadamu hata wakiwa nje ya maji" anasema Mr Whittall.

Mamba anauwezo mkubwa wa kutulia sehemu moja kwa muda mrefu bila kugundulika na myama yoyote hivyo kumtambua inakuwa ni vigumu hiyo ni kutokana na maumbile yao yalivyo na hukimbilia ndani ya vichaka au kuingia kwenye nyumba kama hotelini hapo kufuata joto hasa katika kipindi cha mvua na baridi kali na alipenda kukaa chini ya kitanda hicho kwasababu kulikuwa na joto.

Mkurugenzi huyo alilazimika kuwaita wafanyakazi wengine ambao walisaidiana kumuondoa mamba huyo kutoka kwenye chini ya kitanda na kumtupa kwenye bwawa la hoteli hiyo.

Chanzo Kikuu: Daily Mail, imetofasiliwa na Peruzibongo na kuhaririwa na Dotto Kahindi