Picha na maelezo: Rubani wa ndege ya 'British Air' afanya mapenzi na mamia ya watoto Barani Afrika

  Rubani wa British Airways ametumia nafasi yake kudhalilisha mamia ya watoto wasio salama kwenye shule za Afrika na vituo vya kulelea ... thumbnail 1 summary
 




Rubani wa British Airways ametumia nafasi yake kudhalilisha mamia ya watoto wasio salama kwenye shule za Afrika na vituo vya kulelea watoto, Daily Mail limefichua. 


Ofisa wa Kwanza Simon Wood, mwenye umri wa miaka 54, alidai alikuwa akifanya kazi za kujitolea kwa niaba ya shirika hilo la ndege huku akiwadhalilisha wengi wa wasichana wadogo wakati wa vituo vyake barani Afrika.

Akivalia sare bandia za rubani, alitumia sifa nzuri za shirika hilo - na hata wanasesere waliowekwa nembo za shirika hilo na vitabu vilivyopakwa rangi za shirika hilo - kushawishi watoto kwenye safari za mchana na kwenye hoteli za nyota tano zinazotumiwa na shirika hilo la ndege, ambako aliwadhalilisha.

British Airways sasa inakabiliana na mashitaka yanayoibomoa kwa kiasi kikubwa yaliyowasilishwa na waathirika wake, ambao wanasema kampuni hiyo imeshindwa kuwalinda kutokana na udhalilishaji wake wa kutisha.

Baada ya kuwadhalilisha watoto kwa miaka 15, rubani huyo anayelipwa Pauni za Uingereza 100,000 kwa mwaka hatimaye aliacha pale aliposhitakiwa kwa mashitaka tofauti ya kushiriki ngono na watoto nchini Uingereza.

Siku kadhaa baada ya kufikishwa mahakamani mjini London mwezi uliopita akishitakiwa kwa makosa hayo, Wood alijitupa chini ya treni.

Mwendesha mashitaka Peter Zinner alisema: "Upande wa mashitaka unasema kwamba Wood alikuwa amepotosha kwa kina na kuwahonga watu ambao alitumia uwezo wake wa kuruka kwenda sehemu nyingine za dunia kufanya makosa ya kujamiiana dhidi ya watoto."

Maofisa nchini Kenya wamewatambua takribani watoto 15, wote wanaaminika kuwa wasichana wenye umri wa kati ya miaka mitano na 11, ambao Wood aliwadhalilisha - na kusema wanahofia kuna mamia zaidi.

Wakati British Airways imeanzisha uchunguzi wa kimataifa kuhusiana na tuhuma hizo za 'kushitusha', maswali yameulizwa kuhusiana kwanini rubani huyo - ambaye alikamatwa baada ya shambulio lisilo sahihi kwa msichana wa miaka minane mwaka 2000 - aliruhusiwa tena kufanya kazi karibu na watoto."

Vyanzo vya upande wa mashitaka vilisema vinahofia rubani huyo anaweza kuthibitisha kuwa miongoni mwa wahalifu wa makosa ya kujamiiana.

Katika utumishi wake wa miaka 16 akiwa British Airways, Wood alichagua safari zisizo maarufu ndani na nje ya Afrika Mashariki, akitumia kukaa kwake huko kuwinda watoto wasio salama katika mitaa ya ovyo.

Mawasiliano yake ya kwanza na watoto yanayofahamika katika Afrika yalifanyika mwaka 2001 pale alipoanza kutembelea kituo cha kulelea watoto kilichoko eneo la Karen huko Nairobi, mji mkuu wa Kenya.

Wakati wa Pasaka 2002, alikuwa miongoni mwa wafanyakazi 20 kutoka ndege mbili za British Airways ambao walijitolea kutumia mapumziko hayo na vijana hao wa Kenya, kukijaza kituo hicho kwa zawadi lukuki, dawa na michango iliyochangwa kutoka Uingereza.

Alilieleza shirika la habari la Uingereza la Press Association, ambalo liliripoti safari hiyo: "Tunacheza, kuimba, kufanya kazi mbalimbali na kwa ujumla kuwaburudisha. Tumekuwa karibu mno na watoto hao."

Kwa uhalisia Wood alikuwa akitumia hadhi kubwa ya sare zake za urubani kuweza kuwafikia watoto kwa malengo ya kuwadhalilisha.

Matukio mengi ya hivi karibuni ya udhalilishaji yametokea wakati wa kituo chake Uganda, kituo cha mwisho cha safari yake ya kawaida, kutoka ambako alivuka mpaka huo kwenda nchini Kenya kuwalenga watoto walioko katika mitaa ya ovyo na yatima.

Maofisa nchini Kenya wanasema, alidai alikuwa mshirika wa 'mpango wa British Airways wa uhusiano wa jamii' wakati akiingia kwenye vituo vya kulelea watoto na mashule.

Kama mameneja wakilalamika kuhusu tabia yake, Wood alifungua malalamiko rasmi kwa polisi kwamba wafanyakazi waliohusika walikuwa wakiiba kutoka kwenye nyumba za watoto hao, na takribani mameneja wawili walikamatwa kuhusiana na madai hayo.

Wood kwanza alifikishwa polisi pale alipotuhumiwa kwa tukio la shambulio dhidi ya binti wa miaka minane. Alikutana na binti huyo wakati akijitolea kwa maradhi ya Kisukari nchini Uingereza, akisindikiza watoto wadogo katika safari ya kwenda North Yorkshire mwaka 2000.

Wood alikamatwa kuhusiana na ubakaji, lakini - kama ilivyokuwa kwa skendo la Jimmy Savile - Waendesha Mashitaka wa Mahakama Kuu waliamua hakukuwa na ushahidi wa kutosha kumtia hatiani. Aliruhusiwa kuendelea na kazi yake British Airways na, akaendelea na kazi yake ya kujitolea kwa watoto.

Mama wa mmoja wa waathirika hao wadogo alieleza binti yake alidhalilishwa kwenye hoteli moja ya nyota tano inayotumiwa na wafanyakazi wa British Airways mjini Nairobi.

Alisema kwamba baada ya kumkopesha pesa Wood alimdanganya kumwezesha kumpeleka binti huyo wa miaka mitano kwenye hoteli ya Nairobi Intercontinental.

"Nilimwamini kupita kiasi sababu alionekana mwema sana na mkarimu. Nilimwamini kwa kila kitu, hata kwa binti yangu," alisema.

Msichana huyo, sasa miaka 14, anahangaika shuleni na amekuwa akitokwa machozi na kutengwa. Alitishia kujiua kuepuka aibu na maumivu aliyosababishiwa na Wood.

Pale mashaka yalipoibuka kuhusu Wood nchini Kenya, moja ya shule ziliwasiliana na kampuni ya wanasheria Uingereza, ambayo mfanyakazi wake alisafiri kwenda Kenya akiwa na mtazamo wa kuanza hatua za kisheria dhidi ya Wood na British Airways.

Lakini walipobaini ukubwa wa makosa ya kujamiiana ya Wood dhidi ya watoto hao walipeleka suala hilo kwa polisi wa Uingereza.

Kufuatia kutonywa, maofisa wa Uingereza walimkamata tena Julai 18 kwenye maegesho ya magari ya wafanyakazi wa British Airways katika uwanja wa Heathrow kuhusiana na shambulio la mwaka 2000.

Walipopekua kompyuta zake za mapajani, walikuta picha chafu za vijana wa Kiafrika. Wakati wa msako wa polisi wa gari la Wood sare kadhaa za shule zilikutwa humo, Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Westminster ilielezwa.

Mwendesha Mashitaka Zinner alisema: "Kompyuta yake inashikiliwa na ushahidi ulipatikana kuonesha kwamba alitembelea mitandao kadhaa ya udhalilishaji dhidi ya watoto."

Wood alifikishwa mahakamani Agosti 16 akishitakiwa kwa kumiliki picha chafu na shambulio lisilo sahihi kwa mwanafunzi wa kike mwenye miaka minane.

Aliachiwa kwa dhamana kwa sharti la kusalimisha pasipoti yake lakini siku mbili baadaye alijitupa chini ya treni lililo kwenye kasi karibu na nyumbani kwake huko Potters Bar, Hertfordshire.

Waendesha mashitaka walitangaza Jumatano iliyopita kwamba kutokana na kifo chake, walikuwa wanafanya taratibu za kusimamisha kesi hiyo.

Jennifer Swiddon, anayemwakilisha Wood, alisema kwamba mteja wake alikusudia kukana mashitaka yote dhidi yake kabla ya kifo chake.

Kabla ya kifo chake, Wood alikuwa amehamisha Pauni za Uingereza 64,000 kwenda kwa wawakilishi wake wa kisheria barani Afrika.

Familia ya kaka zake Wood, Nicholas, miaka 52, na Anthony, miaka 51, zilisema ulikuwa 'wakati mgumu kwa familia nzima' na kukataa kuzungumzia suala hilo

Chanzo: Thechoice