Picha: Twiga avamia waendesha baiskeli na kuvunjavunja baiskeli yao, walikuwa wakimpiga picha

Waendesha baiskeli wawili wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kujiingiza katika mchezo wa hatari wa paka na panya mbele ya mnyama mweny... thumbnail 1 summary
Waendesha baiskeli wawili wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kujiingiza katika mchezo wa hatari wa paka na panya mbele ya mnyama mwenye mateke makali Twiga.
Waendesha baiskeli hao walipatwa na kadhia hiyo waliposimama kumpiga picha Twiga wakati wa matembezi yao kwenye hifadhi ya Groenkloof Nature Reserve huko Pretoria, nchini Afrika Kusini.
Cha kuchekesha ni pale mmoja wao alipoanza kuzunguka miti akijificha asipewe teke na Twiga huyo lakini hata hivyo twiga alifanikiwa kuwaonjesha adabu kwa kuikanyaga kanyaga baiskeli yao na kisha kuondoka zake. 

Funzo: Twiga ni mrembo lakini kumbe hapendi kupigwa picha bila idhini yake :-)

Chanzo: Beeld