Picha za ushahidi wa Simba wanaopanda miti Mikumi NP

Wakati wa shughuli zangu Mkoani Morogoro miaka kadhaa iliyopita, siku moja nilitamani sana kufika Ziwa Manyara kuwaona simba wanaopanda mit... thumbnail 1 summary
Wakati wa shughuli zangu Mkoani Morogoro miaka kadhaa iliyopita, siku moja nilitamani sana kufika Ziwa Manyara kuwaona simba wanaopanda miti, nilipiga picha ya umbo lao na namna wanavyoweza kupanda miti na kuifanya hifadhi hiyo kuwa na sifa ya kipekee nchini.

Hivyo nilifungasha safari hadi Manyara na kujionea maajabu hayo. Lakini nilichokiona miaka hiyo Manyara hivi karibuni nimekiona tena kwenye hifadhi ya taifa ya Mikumi, kimenifurahisha na kunifanya nikuhabarishe na wewe kwamba kizazi kipya cha simba wa mikumi nao wanapanda miti.

Kama mawazo yako yanakutuma kupanda mtini kama njia ya kumkimbia simba wa Mikumi atakaekuvamia, pole ndugu, atakufuata juu kwa juu.


Kwa wale akina Thomaso, ambao hawaamini bila kuona wala kugusa, nimekuletea picha 10 zikionyesha simba waki-enjoy na kufanya madoido kadhaa juu ya mti
 www.tabianchi.blogspot.com