Pinda: Nyuki njia mbadala ya kumaliza tatizo la ajira kwa vijana

WITO wa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wa kuitaka jamii kujikita katika ufugaji Nyuki kwa lengo la kujikwamua ... thumbnail 1 summary
WITO wa waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wa kuitaka jamii kujikita katika ufugaji Nyuki kwa lengo la kujikwamua kiuchumi umeanza kupata mafanikio.


Mafanikio hayo yamejitokeza kupitia Asasi ya kiraia ijulikanayo kama Makete Poverty Alleviation (MAPAFO) iliyopo Wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ambapo asasi hiyo imeanza kunufaika na mafunzo ambayo yanatolewa na serikali kupitia wakufunzi idara ya Nyuki na mazingira.

Kwa mujibu wa afisa nyuki wa wilaya ya Ludewa Obothe Msemakweli, Mafunzo hayo ya siku tatu kwa wanachama 15 wa asasi hiyo, yamelenga kuimarisha mradi walionao katika kuendeleza sekta ya ufugaji Nyuki kitaalamu na kuitoathiri mazingira katika maeneo ya mradi.

Huo ni Mpango wa serikali katika kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja na pia katika makundi lengo likiwa ni utekelezaji wa  kauri mbiu ya Taifa ya  Matokea makubwa  sasa  (BRN), ambapo katika kutekeleza hilo serikali imeanza kutoa mafunzo hayo ili kuinua kipato cha wakulima na wafugaji hamasa kubwa ikielekezwa katika kilimo,ufugaji nyuki na  mazao ya chakula na biashara.

Pamoja na kuwepo  kwa mafanikio hayo , wito umetolewa  kwa Asasi nyingine kutobweteka na  washiriki wametambua ni njia ipi inayofaa katika kuboresha zao la asali.

Katika Asasi ya MAPAFO miche ya mikaratusi zaidi ya 8,000 imewatikwa kwaajili ya kupandwa msimu huu, na miti ya matunda  zaidi ya 1,000 aina mbalimbali  ili kutekeleza lengo la utunzaji na uhifadhi wa mazingira.