Na Walter Mguluchuma-Mpanda
Serikali
ya wilaya ya Mpanda imetangaza kuwahamisha wananchi wote wanaoishi katika
Kitongoji cha Kamama Kata ya Mpandandogo na kukifunga kijiji cha bugwe
kilichopo katika Tarafa ya Kabungu wilayani hapa kutokana na uharibifu
mkubwa wa mazingira.
Uharibifu huo unaofanywa na wafugaji na shughuli za
kilimo na kusababisha uharibifu mkubwa wa msitu wa katuma ambao ndio
chanzo kikuu cha mito mingi katika ukanda wa ziwa Tanganyika
Kauli hiyo imetolewa hapo juzi na mkuu wa wilaya ya Mpanda Paza
Mwamlima wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake
Mwamlima alisema zoezi hilo la kuwahamisha watu waliovamia mistu
hiyo limeanza hapo septemba
14 na litadumu kwa muda wa siku kumi na nne na linawashirikisha Kamati ya Ulinzi
na Usalama wilaya, watumishi kutoka ofisi ya Ardhi
na Maliasili pamoja na Viongozi wa Vijiji husika.
Alifafanua
kuwa uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mpanda umeamua kuwahamisha wananchi wa Kitongoji Kamama
kutokana watu hao
kuvamia msitu unaotenganisha
Kata ya Mpanda Ndogo na makazi
ya wakimbizi ya Mishamo eneo ambalo lilikuwa limetengwa kwa ajiri ya shughuli
za uwekezaji
Alisema eneo hilo lenye jumla ya hekari 46,000 pia lilikuwa
limetengwa kwa ajiri ya ujenzi wa kambi ya jeshi la kujenga Taifa na
Shughuli za kilimo kwa vikundi vya vijana
Alieleza
kuwa zoezi hilo la kuwahamisha watu hao litafanyika
kwa kuwaelimisha kwanza wananchi hao ili waweze kutambua umuhimu wa
misitu na tayari eneo la kuwahamishia limeisha andaliwa katika kijiji
cha jirani kinanacha itwa Vikonge katika kata ya Mpanda Ndogo
Kwa upande
wa Kijii cha Bugwe Mwamlima alisema uongozi wa Wilaya unawasiliana na
ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ili iweze kutowa
kibali cha kukifunga kijiji hicho kwani Wizara hiyo ndio yenye mamlaka ya
kukifunga au Kukifunga Vijiji hapa Nchini
Alifafanua
kuwa kKjiji hicho ndicho kinachozungukwa na msitu ambao ndio chanzo cha mito yote muhimu
iliyoko katika ukanda wa
Ziwa Tanganyika ambapo mito
mingi imeanza kukauka kutokana na shughuli zinazofanywa za kibinadamu
Uharibifu
huo wa msitu wa Bugwe tayari umeisha anza kuathiri wanyama katika Hifadhi ya
Taifa ya Katavi kutokana na
kukauka kwa mto Katuma unao peleka maii katika mto wa Sitalike ulioko katika
hifadhi ya Katavi kukauka na kusababisha vifo vya Mamba na Viboko ambapo chanzo cha mto huo ni msitu wa
Bugwe
Alisema kutokana na hari hiyo uongozo wa Wilaya umeamua kuinusuru
hari hiyo na kuanzia sasa maeneo yote ya
Hifadhi ya misitu yatawekewa mabango yanayo kataza watu kufanya shughuli za
kibinadamu katika misitu