MENEJA wa Kampuni ya kuhudumia ndege, abiria na
mizigo katika viwanja vya ndege (Swissport), Gaudence Temu, amesema wamejipanga
kiusalama muda wote ili kuzuia matukio mbalimbali ya kigaidi yasitokee kwenye
viwanja vya ndege wanavyotoa huduma.
Temu alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana
alipozungumza na Tanzania Daima juu ya maendeleo ya kampuni yake kwa kipindi
cha miezi sita.
Alisema kwa kushirikiana na maofisa usalama wa
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege wanahakikisha usalama unakuwepo kwa abiria wao kwa
kipindi chote.
Katika hatua nyingine, alisema wanakabiliwa na
changamoto kubwa ya miundombinu kutokana na abiria na ndege kuongezeka na
miundombinu ya viwanja hivyo kuendelea kuwa ya zamani.
Hata hivyo, aliishukuru serikali kwa kuendelea na
ujenzi wa Terminal III, hivyo anaamini usumbufu huo utakwisha.
Chanzo: Tanzania Daima