Tanzania yasaini mkataba wa huduma za Usafiri wa Anga na Singapore

Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (kushoto) na Waziri wa Uchukuzi wa Singapore, Mhe. Lui Tuck Yew (kulia),... thumbnail 1 summary
photo (2)
Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (kushoto) na Waziri wa Uchukuzi wa Singapore, Mhe. Lui Tuck Yew (kulia), wakisaini Mkataba wa Huduma za Usafiri wa Anga kati ya Tanzania na Singapore kwenye ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (International Civil Organization – ICAO), jijini Montreal, Canada mwanzoni mwa wiki.
photo (3)
Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (kushoto) na Waziri wa Uchukuzi wa Singapore, Mhe. Lui Tuck Yew (kulia), wakibalishana  Mkataba wa Huduma za Usafiri wa Anga kati ya Tanzania na Singapore waliousaini mwanzoni mwa wiki jijini Montreal, Canada.

Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe (MB) na Waziri wa Uchukuzi wa Singapore, Mhe. Lui Tuck Yew, wamesaini Mkataba wa Huduma za Usafiri wa Anga kati ya Tanzania na Singapore. Mkataba huo umesainiwa kwenye ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (International Civil Organization – ICAO), jijini Montreal, Canada. Mhe. Mwakyembe yupo Canada kuhudhuria Mkutano Mkuu wa ICAO ulioanza tarehe 24 Septemba, 2013.

Kusainiwa kwa Mkataba wa Huduma za Usafiri wa Anga ni utekelezaji agizo la Marais wa nchi hizi mbili lililotolewa mwezi Juni, 2013 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Singapore. Wakati wa ziara ya Mhe. Rais nchini Singapore, Marais wa nchi hizi mbili waliziagiza Wizara za Uchukuzi kukamilisha Mkataba huo mapema.

Kusainiwa kwa Mkataba huo kunawezesha mashirika ya ndege ya nchi hizi mbili kuanzisha huduma za usafiri wa anga na hivyo kutoa fursa kwa wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kusafiri moja kwa moja kati ya nchi hizi mbili. Hatua hii itatoa unafuu kwa wasafiri kwa kupunguza muda na gharama za safari. Mkataba huo pia unatarajiwa kufungua fursa za kiuchumi na kijamii kati ya nchi hizi ikiwemo utalii na biashara.

Dar es Salaam yetu