Tembo 81 wauawa tena kwa sumu Zimbabwe

Maafisa wa wanyama pori nchini Zimbabwe wamesema kuwa takriban tembo 81 wameuawa kutokana na sumu iliyomwagwa katika eneo la malisho ya t... thumbnail 1 summary
Maafisa wa wanyama pori nchini Zimbabwe wamesema kuwa takriban tembo 81 wameuawa kutokana na sumu iliyomwagwa katika eneo la malisho ya tembo hao.
Tangazo hilo linajiri baada ya maafisa kuzuru mbuga ya wanyama pori ya Hwange mwishoni mwa juma lililopita.
Sumu hiyo ambayo hutumiwa katika migodi ya dhahabu ilimwagwa katika eneo hilo na wawindaji haramu.
Tayari wawindaji haramu 9 wamekamatwa. Zaidi ya ndovu 40 walipataikana wameuawa katika mbuga hiyo mwezi uliopita.

Chanzo: BBC