Shirika
la habari la NBC limejikuta katika lawama nzito baada ya kurusha kipindi
kinachoonyesha namna wawindaji wa wanyama wanavyoua wanyama huku wakifurahia na
kujipngeza kwa kunywa pombe kwa kufanya mauaji hayo.
Katika
kipindi hicho kinachoitwa Under Wild Skies, Tony Makris kutoka National Rifle Association
anaweka wazi namna anavyofurahia kuua wanyama maneo ambayo yameambatana na
vitendo vya kumuua tembo kwa kumpiga risasi kisha kupiga nae picha na baadae
kufungua shampeni kujipongeza.
Kitendo
hiki kimewakera wengi na hakika kinapaswa kupigwa marufuku kama nia ya dhadi ya
kupambana na mauaji ya wanyama Afrika imekusudiwa.
Tazama video ya kipindi chenyewe ambayo imewekwa na geographic
Wakati Afrika ikiwa katika hatari ya kupoteza tembo wake lakini vitendo kama hivyo vya kuuza tembo kwa kuwafurahisha wachache vinaendelea kushamiri, katika kipindi cha nyuma niliwahi kuleta makala iliyoonyesha wazungu wakiwa wameua twiga ili wapige nae picha tu kitu ambacho si cha kiungwana hata kidogo.