Wachina wanaokwenda Kenya sasa kutumiwa ujumbe wa onyo la ujangili 'Poaching warnings SMS'

Ubalozi wa China nchini Kenya umeanza kutuma ujumbe wa kuzuia ujangili kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneo (SMS) kwa kila mgeni atakaeingi... thumbnail 1 summary
Ubalozi wa China nchini Kenya umeanza kutuma ujumbe wa kuzuia ujangili kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneo (SMS) kwa kila mgeni atakaeingia Kenya kutoka China ikiwa ni hatua yake ya kujisafisha na sifa ya taifa hilo kujihusisha na ujangili na biashara ya nyara za tembo na faru.
Counselor wa Ubalozi wa China nchini Kenya Cao Xiaolin amesema wageni wa kutoka Uchina watatumiwa ujumbe huo wa na kuonywa kujihusisha na ujangili hasa kufuatia wengi kutuhumiwa kwa kufanya biashara hiyo.
Pamoja na China kuwa chanzo kikubwa cha mapato kupitia sekta ya utalii na kusadia shughuli za utunzaji wa mazingira lakini jambo la kuhusishwa na vitendo vya ujangili limeendelea kuwachefua. Wengi wakidhani huenda wanafanya mtindo wa panya wa kung'ata na kupuliza.
Counselor huyo anasema kuongezeka kwa taarifa zinazotuhumu uchina kujihusisha na biashara ya nyara hizo si tu kunachafua sifa ya nchi yao bali kunadhoofisha mahusiano mema yaliyopo baina ya nchi za Afrika na China.
Kiongozi huyo pia alikabidhi vifaa vya kupambana na ujangili ambapo alitoa vifaa vya 20 vya GPRS, darubini 20, kamera 20, tochi 50 na magari mawili.
China na mataifa mengine ya bara la Asia wamekuwa wakilaumiwa kwa kushindwa kusitisha biashara ya pembe za ndovu na faru, hasa kutokana na wafanyabiashara wkubwa kuhusishwa na kufadhili shughuli za ujangili barani Afrika.