WADAU KUKUTANA KUJADILI RASIMU YA SHERIA NA MUUNDO WA MAMLAKA YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI UTAKAOANZA NOVEMBA 2013

Wizara ya Maliasili na Utalii inakutana na wadau wa uhifadhi na matumizi endelevu ya wanyamapori kujadili rasimu za Sheria na Muundo wa Maml... thumbnail 1 summary
Wizara ya Maliasili na Utalii inakutana na wadau wa uhifadhi na matumizi endelevu ya wanyamapori kujadili rasimu za Sheria naMuundo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori pamoja na marekebisho ya sheria ya uhifadhi wa wanyamapori.

Mkutano huo utafanyika kwa siku mbili Septemba 19 – 20, 2013 (Alhamisi na Ijumaa) katika Ukumbi wa Baraza la Maaskofi jijini Dar es salaam ambapo wadau watapata fursa ya kushiriki na kutoa maoni kwenye rasimu ya mapendekezo ya kuundwa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori.

Wakati wa mkutano huo, Wizara itatoa mrejesho wa maoni mbalimbali yaliyotolewa na wadau katika vikao vya awali vilivyofanyika kuanzia mwezi Julai, 2012.

Takriban washiriki 70 wamealikwa kushiriki katika mkutano huo ambao utafunguliwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. M. K Tarishi Septemba 19, 2013.

Mchakato huu wa uundwaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori unatekeleza agizo la Sheria ya Wanyamapori Na. 5 ya Mwaka 2009, ambayo inaitaka Wizara kuanzisha mamlaka hiyo. Mchakato huo umepangwa kukamilishwa Novemba, 2013 baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha sheria husika.

C.K. Rumisha
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII