Wanasayansi: Kutakuwa na jua kali litakalowaangamiza watu wote duniani baada ya miaka bilioni 3.5

Mwisho wa dunia kwa mujibu wa wanasayansi bado sana. Maisha duniani yataendelea kuwepo kwa miaka bilioni 3.5 mingine. Baada ya hapo w... thumbnail 1 summary

Mwisho wa dunia kwa mujibu wa wanasayansi bado sana. Maisha duniani yataendelea kuwepo kwa miaka bilioni 3.5 mingine.


article-0-00530FDC00000258-292_634x502
Baada ya hapo wanasayansi wanaamini jua litakuwa kali kiasi ambacho hakuna kiumbe kitakachoweza kuishi. Tangu iwepo, sayari ya dunia imekuwa kwenye umbali sahihi kutoka kwenye jua kiasi cha kuifanya iwe kuwa na maisha.
Wanasema tatizo ni kwamba nyota zimeendelea kuchemka kadri muda unavyoenda na zikiendelea kutoa joto zaidi, maji ya dunia yataendelea kukauka na kupote kabisa. Utabiri huo umetoka kwa wataalam wa chuo kikuu cha East Anglia ambapo mtafiti mmoja wapo, Andrew Rushby amesema baada ya miaka hiyo dunia itakuwe na joto kali kiasi ambapo hata bahari zitageuka kuwa mvuke.
Alisema binadamu watakuwa viumbe wa kwanza kupotea.

Chanzo kikuu: Daily Mail, imeandaliwa na Bongo5