Watu 200,000 duniani watuma maombi kwenda kuishi milele kwenye sayari ya Mars

Mtandao wa bongo5 umeandika habari hii nami naileta kwako. Tiketi ya one way kwenda kuishi kwenye eneo tasa, lenye ardhi ya ajabu, joto lin... thumbnail 1 summary

Mtandao wa bongo5 umeandika habari hii nami naileta kwako. Tiketi ya one way kwenda kuishi kwenye eneo tasa, lenye ardhi ya ajabu, joto linaloweza kugota 150°C, inaweza isiwe na mvuto kwa wengi, lakini mpaka sasa watu laki 2 kutoka nchi 140 duniani wametuma maombi yao kuwa sehemu ya wakoloni wa kwanza kwenda Mars.


Waombaji wamekubali kuishi kwenye sayari hiyo nyekundu kwa maisha yote yaliyosalia na watashutiwa kwenye reality TV show.
article-0-16D5B5EA000005DC-73_634x242

Kampuni ya Uholanzi ya Mars One inajiinda kwenda kwenye sayari hiyo October 2016 kuandaa mazingira na makazi kuwekwa huko mwaka 2018.
article-2259706-16D5B5DE000005DC-319_634x322
Greda itakavyokarabati ardhi kuwezesha watu kuishi Mars

Imesema kuwa mifumo ya kwenda huko itajaribiwa mara 8 kabla haijatumiwa kusafirisha watu na kwamba safari itakuwa salama kuliko ile ya kwenda mwezini.

Chanzo: Bongo5, Chanzo cha awali: Daily Mail