WWF: Wanajeshi vinara wa ujangili, hutumia silaha za kivita kwa kushirikiana na maafisa wa serikali (video)

Documentary iliyoandaliwa na Wildlife World Fund na kupewa jina la  Wildlife crime is dead serious imetaja kuwa majangili wamekuwa wakisamba... thumbnail 1 summary
Documentary iliyoandaliwa na Wildlife World Fund na kupewa jina la Wildlife crime is dead serious imetaja kuwa majangili wamekuwa wakisambaza rushwa kuanzia kwa viongozi wa serikali ngazi za vijiji hadi taifa, huku wakila sahani moja na askari wanyama pori, vigogo serikalini na maofisa katika mamlaka mbalimbali za hifadhi za taifa.

Ripoti hiyo pia umetaja kuwa asilimia kubwa ya majangili ni maaskari na maafisa usalama wa majeshi mbalimbali, ikiwemo polisi, wanajeshi, askari wanyama pori nk, na wengi ni wale waliofukuzwa makazini na wale waliostaafu

Lakini mbaya zaidi katika kipindi mbinu mpya za ujangili zimewekwa bayana na kuonesha ukubwa wa tatizo la ujangili barani Afrika na duniani kwa ujumla.

Idadi ya wanyama kama tembo, chui, rhino inatajwa kupungua na endapo vitendo vya ujangili vitaendelea kuna hatari ya kupotea kabisa kwa wanyama hao duniani

Tazama video hapo chini ikiwa ni awamu ya kwanza la documentary ya Wildlife crime is dead serious.