Zaidi ya abiria 280 wanusurika kifo katika ajali ya ndege

BANGKOK (AP) — Ndege ya abiria ya Thai Airways ikiwa imebeba zaidi ya abiria 280 imepata ajali wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa ... thumbnail 1 summary


BANGKOK (AP) — Ndege ya abiria ya Thai Airways ikiwa imebeba zaidi ya abiria 280 imepata ajali wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege wa Bangkok na kujeruhi watu 14
Muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea wafanyakazi wa ndege hiyo walilazimika kuondoa nembo (logo) ya ndege hiyo upande wa mkia na ubavuni ikiwa ni hatua ya kulinda hadhi yake na kutojichafulia jina
Ndege hiyo Airbus A330-300 ilikuwa ikitokea Guangzhou, China na ilipata hitilafu kwenye matairi wakati ikitua kwenye uwanja wa ndege jana usiku, na kwamba abiria wote waliojeruhiwa wamekimbizwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Chanzo: AP