News Update: Katika picha zaidi ya Nyumbu 3000 wamekufa maji Mto Mara

Kutoka katika ukurasa wa mtandao wa Facebook, Mara Triangle imeripoti kuwa takribani nyumbu 3000 wamezama maji jana wakati wakivuka kwenye... thumbnail 1 summary
Kutoka katika ukurasa wa mtandao wa Facebook, Mara Triangle imeripoti kuwa takribani nyumbu 3000 wamezama maji jana wakati wakivuka kwenye mto mara kutokana kasi kubwa na maji na kingo ndefu kwenye mto huo.

 Mizoga ya Nyumbu ndani ya mto Mara
“Tumewaona nyumbu wengi hata asubuhi ya leo (Alhamisi) wakizama katika daraja la Purungat na huenda wanaweza kufa wengi zaidi” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo

Hii ni habari mbaya kwa tukio maalumu la uhamaji wa nyumbu wakiwa wanatokea Maasai Mara nchini Kenya kuja Serengeti Tanzania, lakini kuharibika kwa kingo kunaweza kuwa kumesababishwa na shughuli za binadamu.


Tazama video ya uhamaji wa nyumbu kuvuta Mto Mara