44 wafariki kwenye ajali ya ndege Laos

Abiria wote waliokuwa ndani ya ndege ya LAO wakitokea nchini Laos wamefariki baada ya ndege iliyokuwa imewabeba kuanguka Kusini mwa nchi ... thumbnail 1 summary
Abiria wote waliokuwa ndani ya ndege ya LAO wakitokea nchini Laos wamefariki baada ya ndege iliyokuwa imewabeba kuanguka Kusini mwa nchi hiyo.
Maafisa katika nchi jirani ya Thailand wamesema kuwa ndege hiyo ilianguka ndani ya mto Mekong.
Aidha inaarifiwa kuwa ndege hiyo ilianguka kutokana na hali mbaya ya hewa muda mfupi kabla ya kutua katika uwanja wa Pakse.
Ndege hiyo ilikuwa inatoka katika mji mkuu wa Laos wa Vientiane ilipoanguka asubuhi ya leo.
Msemaji katika wizara ya mambo ya nje Sek Wannamethee alisema kuwa abiria 39 na wafanyakazi 4 walikuwa ndani ya ndege hiyo
Alisema rai watano wa Thailand walikuwa miongoni mwa waliofariki.

Chanzo: BBC/Swahili