Asasi za vijana Tanzania zawataka mataifa kupunguza hewa ukaa kwa maslahi ya vizazi vijavyo

Afisa Mradi wa Norwegian Church Aid, Gilbert Mworia (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa mataifa... thumbnail 1 summary
DSC_1038
Afisa Mradi wa Norwegian Church Aid, Gilbert Mworia (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya umuhimu wa mataifa yote duniani kuafiki kupunguza hewa ya ukaa kwa haraka katika kupambana na mabadiliko ya tabianchi (kushoto) Franscisca Damian Kiongozi wa Msafara wa Mazingira .
DSC_1045
Franscisca Damian Kiongozi wa Msafara wa Mazingira akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
DSC_1058
Mchungaji Eliewaha Herman Msuya akizungumza na waandishi wa habari umuhimu wa mataifa ya dunia kuafikiana kwa haraka juu ya kupunguza hewa ukaa kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
DSC_1063
Baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari mbali mbali nchini waliohudhuria mkutano wa vijana kutoka taasisis mbalimbali za kidini juu ya mabadiliko ya tabianchi.
Na MOblog Team
VIJANA Kutoka taasisi za kidini, asasi za kiraia na makundi mbali mbali ya vijana wameyataka mataifa yote duniani kuafiki kupunguza hewa ukaa kwa haraka katika harakati ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Vijana hao kutoka taasisis mbalimbali wanasema kwamba hawaafiki nchi yoyote kupewa kibali cha kuendelea kuzalisha hewa ukaa kwenye anga, ambapo madhara yake yanaweza kudumu kwa miaka mingi.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba wa vijana wa taasisi mbali mbali za kidini hapa nchini jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Afisa Mradi wa Shirika la Norwegian Church Aid, Gilbert Mworia amesema kwamba wanayasihi mataifa yote kuondoa ruzuku haraka kwenye nishati zitoazo hewa ukaa.
“Tunaamini kwamba ‘Green Fund’ itatakiwa kutoa msaada na si mikopo kwa nchi zinazoendelea kwa ajili ya kusaidia jamii kuhimili mabadiliko ya hali ya tabianchi,’ amesema Mworia.
Chanzo: Moblog