IJUE BUSTANI YA WANYAMAPORI YA RUHILA

Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila ina ukubwa wa Hekta 600 na ipo umbali wa kilometa saba Kaskazini magharibi mwa Manispaa ya Songea.Bustani... thumbnail 1 summary
Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila ina ukubwa wa Hekta 600 na ipo umbali wa kilometa saba Kaskazini magharibi mwa Manispaa ya Songea.Bustani ya Ruhila ilianzishwa mwaka 1973 chini ya usimamizi wa Mkoa wa Ruvuma na sasa iko chini ya Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania(TWPF).

Ndani ya bustani hiyo kuna wanyama wa aina mbalimbali wakiwemo Pongo,Pundamilia,Fisimaji,Nyani,Tumbili,Kakakuona na Kobe.Pia bustani hiyo ni makazi ya reptilia na ndege wa aina mbalimbali.

Ndani ya Bustani ya Ruhila kuna aina mbalimbali za mimea ya asili ikiwa ni pamoja na miombo,mininga,mikusu,migunga,miwanga,mizambarau,mirama,mitunduru,misasa,miviru na mikuyu.

NAMNA YA KUFIKA RUHILA

Bustani ya Ruhila inaweza kufikika kwa kutumia barabara ya Songea-Njombe ambayo ni ya lami na kisha ukifika Msamala unafuata barabara ya vumbi ambayo iko kushoto ukitoka Songea au kulia ukitokea Njombe hadi kikosi Dhidi ujangili Kanda ya Kusini ilipo Bustani ya Ruhila.

MALAZI

Malazi kwa wageni yanapatikana katika Manispaa ya Songea.Vilevile wageni wanaweza kuweka mahema ya muda katika maeneo yaliotengwa ndani ya bustani hiyo.

WAKATI WA KUTEMBELEA RUHILA

Unaweza kuitembelea bustani ya Ruhila wakati wote wa mwaka kwa sababu inafikika kirahisi.

SHUGHULI ZA UTALII ZINAZOFANYIKA RUHILA

Ndani ya bustani ya Ruhila,mgeni anaweza kufanya utalii wa kutembea kwa miguu,kupiga picha,pamoja na kuangalia wanyama na ndege.Pia utalii wa kuweka kambi (Camping) na kufanya mapumziko ya mchana (picnic) hufanyika ndani ya eneo maalumu kwa ajili ya shughuli hizo.

VITU AMBAVYO MGENI ANASHAURIWA KUBEBA ANAPOTEMBELEA RUHILA

Wageni wanaotembelea Bustani ya Ruhila wanashauliwa kwenda na :
- Vifaa vya picnic,kamera na vitabu vya kutambua wanyama na
Ndege.
- Vifaa vya kupigia kambi (camping) kwa wale watakaopenda
kulala
Wanashauliwa kuwa na vifaa vya kuweka kambi.

TOZO YA KIINGILIO

i.Raia
- Watu wazima Shilingi 2,000
- Watoto kati ya miaka 6 hadi 16 Shilingi 500
- Watoto chini ya miaka 6 bure

ii. Wageni Wakaazi
- Watu wazima Shilingi 5,000
- Watoto kati ya miaka 6 hadi 16 Shilingi 1,000
- Watoto chini ya miaka 6 bure

iii. Wageni
- Watu wazima Dola 10 za Kimarekani
- Watoto kati ya miaka 6 hadi 16 Dola 5 za Kimarekani

iv.Marafiki wa Ruhila
- Kiasi kisichopungua shilingi 50,000 kwa mwaka

MUDA WA KUINGIA NA KUTOKA

Wageni wanaruhusiwa kuingia ndani ya bustani kuanzia saa 1 :00 asubuhi hadi saa 12 :00 jioni.

TARATIBU ZA KUZINGATIA

Unapokuwa ndani ya bustani unatakiwa kuzingatia yafuatayo:

- Wanyama wasisumbuliwe au kupewa chakula
- Takataka zitupwe kwenye mapipa yaliowekwa
- Usianzishe moto wala kutupa ovyo vishina vya sigara
- Usiwinde wala kukamata mnyama au ndege
- Pita katika njia zilizoruhusiwa tu
- Si vyema kusumbua au kubughudhi wageni wengine.


Chanzo: Maliasili zetu