JK kuzindua rasmi Mkoa wa Njombe

 Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuuzindua rasmi Mkoa wa Njombe Oktoba 18 mwaka huu. Mkoa huo, ulianza rasmi shughuli za kiutawala ya M... thumbnail 1 summary
 Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuuzindua rasmi Mkoa wa Njombe Oktoba 18 mwaka huu.
Mkoa huo, ulianza rasmi shughuli za kiutawala ya Mei 2 mwaka jana.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Aseri Msangi, alisema Rais Kikwete anatarajiwa kuwasili mkoani humo Oktoba 17, 2013 akitokea mkoani Iringa.
Alisema uzinduzi wa mkoa huo uliomegwa kutoka katika Mkoa wa Iringa, utafanyika mchana wa Oktoba 18 katika Uwanja wa SabaSaba mjini Njombe.
Kwa mujibu wa Msangi, shughuli hizo zitatanguliwa na uzinduzi wa Kiwanda cha chai Ikanga, katika Tarafa ya Lupembe.
Msangi alisema uzinduzi huo utahusisha maonyesho ya shughuli mbalimbali za ujasiriamali.
Alisema uzinduzi huo wa mkoa, utaambatana na ziara ya Rais ya siku tano katika wilaya zote nne za Mkoa wa Njombe.
Chanzo: Mwananchi